Msajili
wa Hazina Dkt. Oswald Mashindano (kushoto) akizungumza na Wenyeviti wa
Bodi za Mashirika ya Umma na Taasisi za Serikali pamoja Watendaji Wakuu
wa taasisi hizo (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kuweka saini mkataba
wa utendaji kazi kwa taasisi hizo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Msajili
wa Hazina Dkt. Oswald Mashindano (wa pili kushoto) pamoja na Mwenyekiti
wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Anne Makinda (wa pili
kulia) wakiweka saini katika mkataba wa utendaji kazi mapema hii leo
jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali
Watu toka Ofisi ya Msajili wa Hazina Bw. Michael John na kulia ni Kaimu
Meneja wa Sheria toka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bi. Martha Charles.
Msajili
wa Hazina Dkt. Oswald Mashindano (wa pili kushoto) akimkabidhi
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Anne Makinda
(wa pili kulia) mkataba wa utendaji kazi mapema hii leo jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu toka Ofisi
ya Msajili wa Hazina Bw. Michael John na kulia ni Kaimu Meneja wa Sheria
toka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bi. Martha Charles.
Msajili
wa Hazina Dkt. Oswald Mashindano (kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi
ya Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) Bi. Gaudensia Kabaka (kulia) wakiweka saini
katika mkataba wa utendaji kazi mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Msajili
wa Hazina Dkt. Oswald Mashindano (kushoto) akimkabidhi Mwenyekiti wa
Bodi ya Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) Bi. Gaudensia Kabaka (kulia) mkataba wa
utendaji kazi mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya Wenyeviti wa Bodi za Mashirika ya Umma na Taasisi za Serikali pamoja
Watendaji Wakuu wa taasisi hizo wakimsikiliza Msajili wa Hazina Dkt.
Oswald Mashindano (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kuweka saini
mikataba ya utendaji kazi kwa taasisi na Mashirika ya Umma mapema hii
leo jijini Dar es Salaam.
Na.Bushiri Matenda-MAELEZO
Ofisi
ya Msajili wa Hazina inasema kuwa Taasisi na Mashirika ya Umma sasa
rasmi kutekeleza mkakati wa utendaji kazi ili kujiendesha na kutoa gawio
kwa Serikali yenye lengo la kuchochea maendeleo kwa taifa na kuendelea
kuboresha huduma bora za kijamii.
Hayo
yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Msajili Mkuu wa Hazina Dkt.Oswad
Mashindano wakati wa hafla ya kutia saini mkataba wa utendaji kazi baina
ya Msajili wa Hazina na baadhi ya Wenyeviti wa bodi na Watendaji Wakuu
wa Taasisi na Mashirika ya Umma nchini.
“Ofisi
ya Hazina inasimamia Taasisi mbalimbali takribani 265, ni vyema Taasisi
hizo kwa kushirikiana kwa pamoja zikasimamiwa vizuri ili kutoa huduma
endelevu na kuchangia katika uwekezaji wenye tija kwa taifa”,alisema
Dkt.Mashindano.
Aidha
alisema kuwa mwaka 2014-2015 Ofisi ya msajili wa hazina walifunga
mkataba naTaasisi na Mashirika ya Umma 71 kati ya 265 ambapo mkataba huo
ulilenga katika maeneo manne ya kiutendaji ambayo ni usimamizi katika
rasilimali fedha , watu, utawala bora na huduma kwa wateja.
Dkt.
Mashindano aliongeza kuwa Katika tathmini ya mkataba uliopita kupitia
nyaraka mbalimbali , uchambuzi umeonyesha kuwa zipo baadhi ya dosari
katika utekelezaji wa makubaliano ya awali ambazo alizitaja kuwa
asilimia 25 ya mpango mkakati waliojiwekea Taasisi na Mashirika
hayaendani na bajeti waliojiwekea.
Pili
malengo yaliyobainishwa na Taasisis hizo hayaendani na mpango kazi ,
maeneo ya ya usimamizi wa rasilimali watu na utawala bado kuna
changamoto, eneo la ukusanyaji mapato katika baadhi ya Taasisi bado ni
ndogo pamoja na eneo la Huduma kwa wateja linahitaji kusimamiwa
ipasavyo na kuwepo kwa baadhi ya Taasisi na Mashirika ya Umma kujaza
matokeo ya kazi ambazo hazipo kwenye utekelezaji wa mapango kazi.
“Katika
utiaji wa sahihi, mkataba huu unaohusisha zaidi ya Taasisi na
Mashirika 30 naamini tutazingatia kutatua changamoto zilizopo na kuweka
mpango wa maendeleo endelevu”, alisisitiza Dkt. Mashindano.
Naye
spika wa bunge mstaafu ambaye pia ni mwenyekiti wa Bodi wa Mfuko wa
bima wa afya Bi. Anna Makinda alitoa neno kwa niaba ya wenyeviti wa
Bodi wa Taasisi na Mashirika ya Umma alisema ni vizuri tukatatua
changamoto zilizojitokeza katika uendeshaji wa mashirika ya Umma ili
yajiendeshe kwa tija na maslahi ya Taifa.
“Watendaji
wakuu wa Taasisi za Umma na wenyeviti wa Bodi tunawajibishwa na
makubaliano haya, tunategemewa sana katika kuwaletea maendeleo wananchi
na Taifa kwa ujumla”, alisema Bi. Makinda.
Aliongeza
kuwa Taasisi za vyuo vikuu vilivyoingia makubaliano haya watawajibika
katika kuwatayarisha vijana katika kuliletea Taifa maendeleo.
Wenyeviti
wa Bodi na watendaji wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma wanatakiwa
kufanya kazi kwa kuzingatia miongozo iliyopo taratibu na Sheria zilizopo
kwa kushirikiana na Ofisi ya Hazina ili kuleta tija kwa watumishi
wengine katika Taasisi za Umma.
Mbali
na majukumu iliyonayo Ofisi ya Msajili wa Hazina pia inasimamia katika
masuala yote ya uwekezaji nchini, mitaji, malipo mbalimbali ikiwemo
mishahara kwa watumishi wa Umma.
EmoticonEmoticon