Kushoto Naibu Waziri Ofisi ya Makamu
wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Kiongea na vijana katika eneo
la Bunju A Usalama, kuhusu Karavati (hawapo pichani) ambalo lilikuwa ni moja ya
kero ya kuchangia mafuriko katika eneo hilo hasa katika vipindi vya mvua
kutokana na uchafu wa mazingira uliopelekea karavati hilo kuziba. Naibu Waziri
Mpina ametembelea eneo hilo leo ikiwa ni sehemu ya ufuatiliaji wa utekelezaji
wa magizo aliyotoa kwa sekta husika
wakati wa ziara yake aliyowahi kuifanya katikamaeneo hayo.
Katikati Naibu Waziri Mpina
akimsikiliza katibu wake Bw. Daniel Sagata (kulia) alipokuwa akizungumza kuhusu
sehemu ya ukuta wa kiwanda cha red sea uliobomolewa kupisha maji ya mvua,
wakati wa ukaguzi wa utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa katika ziara yake
alipotembelea katika eneo la keko mwanga mtaa wa Mafuta kushoto ni Bw. Salea
Haffif mwakilishi wa kiwanda cha Red Sea.
Kushoto Naibu Waziri Mpina
akimsikiliza katibu wake Bw. Daniel Sagata
kulia alipokuwa akimuonyesha tuta lililojengwa na kiwanda cha saruji cha
Wazo cha Tegeta Jijini Dar es Salaam, Tuta ambalo lilijengwa baada ya kujengwa mtaro wa
kupitisha maji ya mvua yaliyokuwa yakisababisha kero ya mafuriko kwa wakazi wa
maeneo jirani yaliyotaka na makorongo yaliyochimbwa na kiwanda hicho kwa lengo
la kutafuta maligafi za kutengeneza saruji, kero hiyo inasemekana kupungua
baada ya Naibu Waziri Mpina kuwahai kufanya ziara kiwandani hapo na kutoa
maagizo.
Katika Picha ni sehemu ndogo ya
korongo inayomwaga maji ya mvua na kuingia katika mfereji uliojengwa na kiwanda
cha wazo.
(Pichani) Mtaro wa maji Machafu
uliokuwa ukilalamikiwa na wakazi wa keko mwanga katika mtaa wa Mafuta habari na
Evelyn Mkokoi
EmoticonEmoticon