WAKILI KAPINGA AENDELEA KUAHIDI MAENDELEO

October 08, 2025


📌 *Ndugu.Kapinga awaomba Wananchi Mbuji wajitokeze kwa wingi kupiga Kura Oktoba 29*


📌 *CCM yaendelea Kunadi Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka2025-2030*


📌 *Wananchi wa Mbuji waahidi kuipigia Kura CCM za Kishindo Oktoba 29*


🔷Mgombea Ubunge Jimbo la Mbinga Vijijini kupitia tiketi ya CCM *Wakili.Ndugu.Judith Kapinga* leo tarehe *08 Oktoba,2025* ameendelea na Ziara yake ya Kampeni ya kuomba Kura za CCM Kata ya Mbuji-Tarafa ya Mbuji.*Ndugu,Kapinga* ametembelea Vijiji vya Mahilo Asili,Mawono,Mbuji na Kilanga Juu✍️.

🔷Katika Ziara hiyo, *Ndugu.Judith Kapinga* amewashukuru Wananchi wa Vijiji hivyo kwa kuhudhuria Mikutano ya Kampeni,lakini akapokea Changamoto mbalimbali za Maendeleo katika Kata hiyo ya Mbuji na amewaahidi Wananchi kwenda kuzishughulikia iwapo atachaguliwa kuwa Mbunge.Mgombea *Ndugu.Kapinga* amewaomba Wananchi wa Mbuji wajitokeze kwa wingi kupiga Kura *Oktoba 29* ,kwa kuwachagua *Ndugu.Dkt.Samia Suluhu Hassan* -Mgombea Urais, *Ndugu.Balozi,Dkt.Emmanuel Nchimbi* -Mgombea mwenza, *Ndugu.Judith Kapinga* -Mgombea Ubunge na *Ndugu.Martin Ndomba* -Mgombea Udiwani wa Kata ya Mbuji✍️.

🔷CCM kupitia Katibu wake *Ndugu.Ally Simba* Katibu wa CCM Wilaya ya Mbinga ameendelea kunadi  Ilani ya CCM ya Uchaguzi ya Mwaka 2025-2030,amewaomba Wananchi wa Mbuji kuipigia Kura CCM ifikapo 29 Oktoba.

🔷Kwa niaba ya Wananchi wa Kata ya Mbuji, *Ndugu.John Kapinga* amekihakikishia chama Cha Mapinduzi *Oktoba 29* Wananchi watakichagua kwa Kura za Kishindo✍️


         *Imetolewa na Ofisi ya Mgombea Ubunge Jimbo la  Mbinga Vijijini,Leo tarehe 08.10.2025*

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »