EACOP NI MRADI WA KUJIVUNIA DUNIANI – BALOZI SEFUE

October 10, 2025




Na Mwandishi Wetu, Tanga


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania TPDC Mhe Balozi Ombeni Sefue amesema kuwa Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki EACOP ni miongoni mwa miradi bora zaidi duniani inayotekelezwa kwa kuzingatia utu haki za binadamu na uhifadhi wa mazingira.


Akizungumza Oktoba 9, 2025 jijini Tanga katika mkutano na waandishi wa habari Balozi Sefue amesema kuwa mradi huo unaotekelezwa kutoka Kabaale Uganda hadi Chongoleani Tanga umefikia hatua kubwa ya utekelezaji na unaendelea kwa kasi nzuri huku ukionyesha mfano wa kuigwa katika usimamizi wa miradi mikubwa ya kimkakati barani Afrika.


Amesema Serikali kupitia TPDC pamoja na wanahisa wenzake wamejipanga kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati na unawanufaisha Watanzania kwa kuzingatia viwango vya kimataifa katika heshima ya haki usalama na utunzaji wa mazingira.

Utekelezaji wa mradi kwa ujumla umefikia asilimia 70 ambapo kazi ya uchomeleaji wa mabomba imekamilika kwa zaidi ya kilomita 946 sawa na asilimia 65.6% ya urefu wote wa bomba huku ujenzi wa bomba ukitarajiwa kukamilika Julai 2026 Serikali ya Tanzania imehakikisha hakuna ucheleweshaji unaosababishwa na changamoto za kifedha kwani fedha zote za utekelezaji zimeshapatikana kwa asilimia 100.


Katika hatua za utekelezaji wananchi 9869 kati ya 9927 waliopisha eneo la mradi wamelipwa fidia kwa jumla ya Shilingi Bilioni 35.06 ambapo mkoani Tanga pekee wananchi 1688 wamepokea fidia ya zaidi ya Shilingi Bilioni 10.49.


Aidha nyumba 340 za makazi mbadala zimejengwa kwa wananchi 294 kati yao 40 kutoka mkoa wa Tanga wamenufaika kwa nyumba 43 mpya.


Kuhusu ajira jumla ya ajira 9194 zimezalishwa ambapo Watanzania 6895 sawa na asilimia 75 wamenufaika moja kwa moja kupitia kazi zenye ujuzi wa kati na wa chini wakati ajira 2299 sawa na asilimia 25 zimenufaisha wataalamu wa ndani katika fani za uhandisi mazingira usalama na maendeleo ya jamii.



Serikali ya Tanzania imekusanya zaidi ya Shilingi Bilioni 70 kupitia vyanzo mbalimbali vya kodi na ushuru unaotokana na mradi huu na matarajio ni kukusanya zaidi ya Shilingi Trilioni 2 baada ya kuanza kwa shughuli rasmi za uendeshaji Katika Jiji la Tanga pekee Halmashauri imekusanya zaidi ya Shilingi Bilioni 2 kutokana na kodi na ada zinazotokana na wakandarasi wa mradi.


Zaidi ya kampuni 200 za Kitanzania zimepata zabuni zenye thamani ya shilingi trilioni 1.325 na fedha hizo zimechochea mzunguko wa uchumi wa ndani kupitia ununuzi wa bidhaa na huduma zinazozalishwa hapa nchini Kupitia utekelezaji wa EACOP barabara zenye jumla ya kilomita 304 zimeboreshwa hivyo kurahisisha shughuli za wananchi na wakandarasi.


Mradi unatekeleza ujenzi wa vituo vitano vya kupoozea umeme vinavyounganishwa na njia za umeme zenye jumla ya kilomita 313.13 hatua itakayowezesha vijiji vingi kuunganishwa na nishati ya umeme kwa mara ya kwanza Aidha mradi unatekelezwa kwa kuzingatia sheria za Tanzania na viwango vya kimataifa ukiweka kipaumbele katika usalama wa wafanyakazi na mazingira.


Miongoni mwa hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kutumia mifumo maalumu ya kuhifadhi joto ndani ya bomba ili kulinda uhai wa viumbe wa ardhini kuhifadhi na kurejesha tabaka la udongo wakati wa ujenzi ili kuruhusu uoto wa asili kurejea kutumia teknolojia ya Horizontal Drilling Direction kuvusha bomba chini ya mito kama Mto Sigi bila kuathiri maji wala bioanuwai kujenga Solar Farms kama chanzo mbadala cha nishati kwa ajili ya mitambo ya mradi.


Mradi wa EACOP pia unashirikiana na taasisi za uhifadhi wa mazingira kama TANAPA NEMC TAWA na TFS kuhakikisha shughuli zote katika hifadhi mbuga na misitu zinafanyika kwa uangalizi mkubwa ili kulinda mazingira.


Katika upande wa jamii mradi umeendelea kujenga uhusiano mzuri na wananchi katika maeneo unakopita ambapo miradi kadhaa ya kijamii inatekelezwa ikiwemo ujenzi wa mtandao wa mabomba ya maji wenye gharama ya shilingi bilioni 4.4 unaowanufaisha zaidi ya wananchi 26000 ujenzi wa Kituo cha Afya katika Kata ya Chongoleani upandaji wa miti milioni 2 ya minazi ujenzi wa uwanja na kituo cha michezo cha timu ya Coastal Union pamoja na mafunzo kwa vijana 800 katika fani za ujenzi mekanika na umeme wa viwandani.


Balozi Sefue amesema licha ya changamoto zilizojitokeza wanahisa wa EACOP wakiwemo TPDC wanaendelea na utekelezaji wa mradi kwa nia ya dhati hadi ukamilike ifikapo mwaka 2026 akisisitiza kuwa EACOP ni mradi wa kielelezo unaoonyesha usimamizi bora wa miradi mikubwa nchini.


Amesema mradi huu ni wa kizazi hiki na vizazi vijavyo kwani unahakikisha Watanzania wananufaika kwa kulipwa fidia kwa haki kujengewa nyumba bora kupewa mafunzo ya kilimo ufugaji na stadi za kazi pamoja na kulindwa mazingira na haki zao za msingi.


Bodi ya TPDC imesisitiza itaendelea kusimamia Menejimenti ya Shirika kuhakikisha ujenzi wa bomba unakamilika kwa wakati na kwa ubora wa hali ya juu huku ikihakikisha Watanzania wanaona matokeo ya moja kwa moja ya uwekezaji huu katika maisha yao ya kila siku.





















Share this

Related Posts

Previous
Next Post »