📌 *Wananchi wamiminika kupata elimu ya Nishati Safi ya Kupikia kwa njia ya vitendo*
📌 *RC Tanga afungua Maadhimisho; atoa pongezi kwa Wizara ya Nishati*
📌 *Ruzuku ya Serikali yawezesha majiko ya gesi ya kilo sita kuuzwa kwa sh. 17,500 katika Banda la REA*
Wizara ya Nishati pamoja na Taasisi zake imeendelea kutumia njia mbalimbali kufikisha elimu ya Nishati Safi ya Kupikia kwa wananchi ambapo safari hii elimu hiyo inatolewa katika Maadhimisho ya Siku ya Chakula duniani yanayofanyika katika Viwanja vya Usagara jijini Tanga.
Akizindua Maadhimisho hayo leo jijini Tanga, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dkt. Batilda Burian ameipongeza Wizara ya Nishati na taasisi zake kwa kushiriki maadhimisho hayo yanayotarajiwa kumalizika Octoba 16 mwaka huu.
Dkt. Burian ameeleza kuwa Nishati Safi ya Kupikia ina mchango wa moja kwa moja katika suala la chakula kwani Serikali kwa sasa inahimiza matumizi ya nishati safi katika kupikia chakula.
Aidha, akiwa katika Banda la Wizara ya Nishati, Dkt. Burian alielezwa na Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati, Omari Khalifa kuwa, Wizara ikishirikiana na taasisi zake, inatekeleza ajenda ya Taifa ya Nishati Safi ya Kupikia ambayo kinara wake ni. Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Khalifa amesema katika maadhimisho hayo Wizara ya Nishati kupitia taasisi yake ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inaendelea kuuza majiko takriban 500 ya Gesi ya kilo sita kwa bei ya Ruzuku ya shilingi 17,500/= kwa wakazi wa Tanga ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa lengo la kufikia asimilia 80 ya wananchi wanaotumia nishati safi ya kupikia ifikapo 2034.
![]() |
EmoticonEmoticon