BENKI YA TIB -TUNAWAJENGEA UWEZO WAJASIRIAMALI KUINGIA KWENYE MASOKO NA KUWEZA KUTAFUTA MITAJI

January 21, 2026



Na Oscar Assenga,TANGA

BENKI ya Maendeleo ya TIB inashiriki maonesho ya tano ya Wiki ya Huduma ya Fedha huku wakieleza kazi yao kubwa kuhakikisha wanaibua wajasiriamali  na kuwajengea uwezo ili waweze kukopesheka na mabenki mengine na kuondokana na changamoto ambazo wanakabiliana nazo .

Hayo yalisemwa leo na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo Tanzania Deogratius Kwiyukwa alisema kazi yao kubwa kuhakikisha wajasiriamali wanaoanza kuwajengea uwezo wa wao kuweza kuingia katika  soko na kuweza kutafuta mitaji katika maeneo mengine


Alisema kwamba vigezo vya upatikanaji wa mikopo ni kama ilivyo kwa taasisi nyengine za kifedha wanaangalia wazo la biashara, kuangalia mradi wake wana kitengo ambacho kinawashauri wafanye ni kwa kupatiwa muongozo ili aweze kukubalika na maneki mengine

Aidha alisema kwamba lengo la benki hiyo ni kuchochea ukuaji wa maendeleo Tanzania na wapo katika uwekezaji kwa kuangalia miradi yote mikubwa iwe ya Serikali na Binafsi kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali katika upande wa maji wanashirikiana na Water Fund kuhakikisha wananchi wanapata maji kwa upana zaidi

Alisema maana yake wanatengeneza impact kwa wananchi ikiwemo wanashirikiana na REA kuhakikisha wanapata umeme hasa vijijini na wale wawezekaji katika nishati ya umeme wanapata fund kwa wakati.



Alieleza baada ya hapo wanaingiza wao kwenye gridi ya Taifa ni Benki ambayo inaanfalia miradi mipana ya Serikali na watu binafasi kuhakikisha zile changamoto ambazo wajasiriamali wanazo wanazifanyia kazi.

Aidha alisema pia benki yao ina tofauti na benki nyengine kwa maana wanachukua muda mrefu katika miradi mpaka miaka 15 pamoja na muda mfupi kutokana na aina ya mradi na wapo kimkakati hatua inayopelekea mchango mkubwa sana kwa maendeleo ya nchi ya Tanzania

“Sisi Benki ya TIB katika kuchochea maendeleo Tanzania na tupo kwenye sekta zote nchini kama wadau wakubwa kuhakikisha nchi hasa katika upande wa viwanda ambavyo pia ndani yake vinachochea ajira wanashirikiana na taasisi mbalimbali binafsi na serikali kuhakikisha wanatengeneza ajira”Alisema

Alisema kwamba na wanapochochea uwepo wa viwanda hata uagizaji wa bidhaa kutoke nje ya nchi unapungua maana yake wataweza kuokoa fedha za kigeni na kuweza kutumia fedha ndani kuliko kuagiza kutoke nje ya nchi.

Katika hatua nyengine alaisema kwa upande wa Kilimo benki hiyo wana dirisha ambalo wanatoa mikopo kuanzia asilimia 3 mpaka 4 kwa wawekezaji ambao wanawezeka kwenye mnyororo mzima wa sekta ya Kilimo.

Alisema kwamba huo ni mchango wao mkubwa kuhakikisha wawekezaji wanaokwenda kuomba mikopo wanapata kwa wakati ili kuenda kuzalisha na kutengeneza ajira mbalimbali kwa Taifa.

Mwisho.


Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »