Katikati Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na
Mazingira Mhe. Luhaga Mpina na Uongozi wa Gereza la keko wakati wa Ziara ya
Naibu Waziri Mpina ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa maagizo yake gerezani keko
ya ujenzi wa miundombinu ya majitaka ambayo ni rafiki kwa mazingira.( Picha na
Evelyn Mkokoi)
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira
Mhe. Luhaga Mpina, Akitoa Maelekezo kwa Uongozi wa Baraza la Taifa la Hifadhi
na usimamizi wa Mazingira (NEMC) Hamlashauri ya Wilaya Ya Temeke, na TANROADS
kuhusu suluhisho la muda na la kudumu la Mfereji wa Mtaa wa Mafuta keko
Gerezani Jijini dar Es Salaam, wenye kuleta kero ya kimazingira kwa wakazi wa
eneo hilo hususan katika kipindi cha mvua.
NA Evelyn Mkokoi- Dar
Es Salaam
Kampuni ijulikanayo kwa jina moja la Red Sea iliyopo katika
Mtaa wa mafuta Keko Gerezaji jijini Dar Es Salaam, Imepewa mwezi mmoja wa
kutakiwa kubomoa ukuta uliojengwa juu ya Mtaro wa maji machafu ambao pia ni
eneo chepechepe, na kusababisha usumbufu kwa wakazi wa maeneo hayo na hatari ya
kupata magonjwa hasa katika kipindi cha mvua.
Akifuatila utekelezaji wa Maagizo ya ziara yake aliyoifanya
tarehe 20 mwezi wa December mwaka jana, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, amesema kuwa ujenzi huo holela,
umekiuka sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake na kumtaka mmiliki wa
kampuni hiyo kubomoa ukuta huo ndani ya siku thelathini na kinyume na hapo
serikali kupitia halmashauri ya wilaya ya Temeke na NEMC itabomoa ukuta ukuta
huo kwa gharama za mmiliki wa kampuni hiyo.
Aidha, Naibu Waziri Mpina Ameitaka NEMC pamoja na Manispaa ya
Temeke kuwasilisha kwake ndani ya siku tatu vibali vilivyomruhusu mmiliki
mwingine wa kampuni ya KOBIL kujenga juu ya mtaro huo, kinyume na hapo hatua
nyingine zitachukuliwa.
Kwa Upande wake Mkaguzi wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS
Bw.Dismas Nyoni, ameeleza kuwa, TANROADS ina mpango wa muda mvupi wa kufanyia
usafi mtaro huo ulioziba na kupita chini ya barabara katika eneo la kilwa road,
na kuzibua mtaro huo ili kuwapunguzia wananchi usumbufu katika msimu wa mvua
zinazokuja.
Wakati huohuo Naibu Waziri Mpina, alitemebelea Gereza la Keko
kujionea utekelezaji wa maagizo yake ambapo awali gereza hilo lilikuwa
likiririsha maji taka katika maeneo ya makazi na kwa hivi sasa gereza la keko
limekamilisha ujenzi wa miundombinu ya maji taka kwa asilimia 80, aliwapongeza
na kuwapa muda wa wiki mbili kumalizia marekebisho yaliyobakia, nae Mkazi wa
eneo la Keko Gerezani Bi ASha Hussein alisema gereza la keko likikamilisha
ujenzi huo wa miundombinu ya maji taka wananchi wataepukana na magonjwa na
watoto watacheza vizuri.
EmoticonEmoticon