Rais wa Jamhuri ya Nigeria Mheshimiwa Bola Ahmed Tinubu , amewasili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati, unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 hadi 28 Januari 2025.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Mheshimiwa Tinubu amelakiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo.
Mheshimiwa Tinubu yuko nchini kwa ajili ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika unaowakutanisha Viongozi wa Nchi za Afrika, wadau wa Sekta ya Nishati na wadau wa maendeleo.
Mkutano huo unalenga kuimarisha juhudi za pamoja katika kukabiliana na changamoto za nishati barani Afrika, sambamba na kupitisha Azimio la Dar es Salaam, linalosisitiza dhamira ya Viongozi wa Nchi na Serikali za Afrika kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika, nafuu, na endelevu barani Afrika.
EmoticonEmoticon