ALIYOSEMA RAIS DKT SAMIA SULUHU WAKATI AKIHUTUBIA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA KUHUSU NISHATI LEO JANUARI 28,2025 JIJINI DAR E SALAam

January 28, 2025


#  Tanzania ni moja ya nchi 12 zinazotekeleza mpango mahususi wa taifa kuhusu nishati ambao utaongeza kasi kuunganisha umeme nchini hadi kufikia asilimia 72 ifikapo 2030.


# Ili kufanikisha mpango huo ndani ya miaka 5 ijayo tutahitaji uwekezaji wenye thamani ya dola za Marekani bilioni 13 ambapo kati ya hizo dola bilioni 5 zitapatikana kutoka sekta binafsi.


# Tumepanga kuongeza uzalishaji wa umeme kutokana na nishati  mchanganyiko ambapo mpaka sasa Tanzania inauwezo wa kuzalisha  megawati 3,431 ambapo asilimia 58 inatokana na vyanzo vya maji, asilimia 35 ni gesi asilia na asilimia 7 inatokana na vyanzo vingine.


# Tumelenga kuongeza megawati 2,463 za nishati kutokana na jua, gesi asilia, upepo na vyanzo vingine ifikapo 2030.


# Tanzania ni kiungo muhimu katika  kuunganisha nchi nyingine za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika na nishati ya umeme,  jambo linalowezesha biashara ya umeme kutoka Afrika Kusini hadi Cairo, Misri.


 #Tayari tumeshaunganisha miundombinu ya umeme na nchi za Burundi,  Rwanda, Kenya na sasa tunaendelea kuunganisha umeme na nchi ya Zambia na Uganda ambapo uwepo wa miundombinu hii utawezesha biashara ya nishati kati ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na SADC.


# Tanzania inayo nafasi ya kuuza umeme, hadi mwezi Novemba 2024 mahitaji ya umeme nchini Tanzania yalikua megawati 1,888 wakati uzalishaji ni megawati 3,431.


# Tumepanga kufikisha umeme kwenye vitongoji vyote, baada ya kufanikiwa kusambaza umeme katika vijiji vyote vya Tanzania ambapo mwelekeo wetu wa sasa ni kuvifikia vitongoji vyote 64,359 ambapo mpaka sasa mpango wetu umeshavifikia vitongoji  32,827 na kazi inaendelea ya kuvifikia vitongoji vilivyobaki.


# Tanzania ina Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya kupikia unaolenga kupandisha kiwango cha matumizi ya nishati safi ya kupikia kutoka asilimia 10 ya sasa hadi asilimia 80 ifikapo mwaka 2030, ambapo mpango mahususi tunaozindua leo utatusaidia kufikia lengo hilo.


*Imeandaliwa na Idara ya Habari Maelezo*

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »