Na Oscar Assenga,TANGA
ASKOFU wa Jimbo Katoliki la Tanga Mhashamu Thomas Kiangio ametaka hatua kali zichukuliwe kwa wanaohusika na kufanya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto ili kukomesha tabia hiyo kwenye jamii.
Aliyasema hayo wakati wa Ufunguzi wa Jubilei Kuu 2025 kwa waandishi wa Habari Jimbo Katoliki la Tanga ambapo alisema kwamba vyombo vya habari havipaswi kukaa kimya badala yake wawe mstari wa mbele kuwafichua wanaofanya vitendo hivyo.
Mhashamu Kiangio alisema kwa sababu pale ambapo vyombo bua habari vinapokaa kimya uovu unapotendeka watakuwa hawana maana yoyote ya uwepo wao kutokana na kusambaza taarifa nzuri kuacha mabaya yatendeka.
“Ukiangalie leo hii watoto wadogo wanahujumiwa wanaingizwa kwenye mifuko ya rambo vyombo vipo wapi na je wanatoa taarifa watoto wanatendwa ukatili wanauwawa wasiokuwa na hatia “alisema
Hata hivyo alisema kwamba wakati mwengine unasikia watoto wamepakiwa kwenye basi wanasafirishwa kuelekea mahali fulani wengine wapo hai wengine wamekufa lakini hawaona hatua wanayotenda kwa watu hao hivyo kuna umuhimu hatua kuchukuliwa.
“Wakati mwengine wanahabari wanatuletea taarifa za uchungu lakini hamtuambii aliyefanya hivyo ni nani na hatua gani zimechukuliwa kuweza kudhibiti vitendo vya namna hiyo kuendelea kwenye jamii”Alisema
Aidha alisema suala hilo lazima wao kama wanahabari walitafakari hasa ikiwa ni hija ya wanahabari kwamba wale ambao wanawatendea mabaya ya kuwaua watu wasiokuwa na hatia wafichuliwa na watoa taarifa kamili na wasitoe nusu nusu ili kuwezesha kukomesha vitendo hivyo
“Wana habari mnakazi kubwa sana na ndio maana Baba Mtakatifu akaifanya siku ya leo duniani ya wana habari kutokana na umuhimu wenu hivyo msiwe waongo mtoe taarifa watuhumiwa wajulikane”Alisema
Ukatili.
Hata hivyo alisema katika suala la ukatili wa watoto Tanga ni ya pili hivyo ni wakati wa wanahabari kubadilika na kuacha kuandika nzuri badaa yake mfichue kwa umakini jambo hilo ili lisiwepo kwenye jamii.
“Salini mkimuomba mwenyezi Mungu awaongoze na kutafuta na kuona maana nyie ni kioo cha jamii lakini tuziombee familia za wana habari wengi wamepoteza maisha kutokana na kuwa wakweli kwa ndio maana wengine wanajificha”Alisema
Dawa za Kulevya.
Askofu Mhashamu Kiangio alisema Tanga inakumbwa na vijana kuingia kwenye dawa za kulevya jambo ambalo linachangia kupoteza nguvu kazi ya Taifa kutokana na kugeuka kuwa tegemezi kwenye familia zao .
“Unapotembea katika maeneo ya Bombo ukipita hapo vijana wenye afya na nguvu wameingia kwenye dawa za kulevya wanaenda kupata tiba hapo serikali inatambua lakini wale wanaowapa wafikie hivyo ni wakina nani? Alihoji Askofu Mhashamu Kiangio.
Askofu huyo alisema kwa sababu wale wanaotumia dawa za kulevya ni ndugu ,kaka na dada zenu hivyo wanahitaji watetezi ambao watawatoa kwenye janga hilo.
Hata hivyo alisema kuna hatari Taifa likaangamia kwa kutokujali wale wanaongaika pale wazazi wao wanafanya nini au ni kuwaacha kupata dawa na kurudi na kumuomba mwenyezi mungu kukomesha matumzi ya dawa za kulevya .
“Fikiria kama ni kaka yako,baba yako,ndugu yako hawezi kupendezwa na jambo hilo hivyo tuwaombee kwenye hija hii mtambua ya kweli msizushie watu huongo”Alisema
Jubilee hii ya mwaka 2025 ina beba ujumbe bila Uchumba Sugu inawezekana jubilee inasema watu wasiishi uchumba sugu ina mana yake kwa wale ambao hawajafunga ndoa.
Aliongeza kwamba katika Jubilei hii ya mwaka 2025 vipo viashiria ambavyo ni msalaba ulipo mbele alama ya ukombozi na kwa kipindi cha miaka 25 ya Jubilee imeona mambo mengi yalitokea mambo makubwa kama vita ya dunia wengi walipoteza maisha.
Alisema pia magonjwa mbalimbali ya kila siku na milipuko na miaka ya karibuni kulitokea ugonjwa wa corona na watu wengi walipoteza maisha na hata sasa kumeweka moto huko Jimbo la Califonia Marekani na katika mawimbi hayo ikaonekana inafaa na kumpendeza Mungu Jubilee ya 2025 ya mahujaji katika matumaini.
Alisema kwa maana yale ambayo yanatuzunguka kwenye maisha yetu ni dhoruba,mahangaikio na changamoro mbalimbal za maisha,magonjwa na machungu mbalimbali na uovu.
Uchaguzi Mkuu.
Askofu Mhashamu Kiangio alisema wanafanya jubilee kumuomba mwenyezi Mungu na kutafakari juu ya Taifa hasa la Tanzania katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wanaomba awape amani na haki ya binadamu iangaliwe kwanza na watu wawe na umoja na mshikamano katika Taifa.
EmoticonEmoticon