Na Oscar Assenga,TANGA
MKUU wa wilaya ya Tanga Japhari Kubecha ameupongeza uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) kwa juhudi za kuhamasisha utalii wa ndani katika mapango hayo huku akitoa rai kwa wananchi ndani na nje ya Mkoa wa Tanga kujenga utamaduni wa kutembelea vivutio vilivyopo ndani ya nchi.
Kubecha aliyasema hayo wakati akizundua kampeni ya Uhamasishaji wa utalii wa ndani katika Mapango ya Amboni Tanga kuelekea sikukuu ya wapendanao inayoadhimishwa kila mwaka February 14.
Kampeni hiyo iliyozinduliwa na Mkuu huyo wa wilaya Januari 26 mwaka huu inaenda na kauli mbiu isemayo “Diko la Amboni Furaha ya Asili,Utajiri wa Urithi ambayo imelenga kuhamasisha utalii wa ndani kukuza uchumi wa wajasiriamali wadogo wadogo mkoani Tanga.
Alisema kwamba wanatambua juhudi za pekee zinazofanywa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kuhakikisha kuwa utalii mambo kale na urithi wa utamaduni unaendelea kuwa kivutio bora cha watalii nchini.
“Kutokana na hili nitoe wito kwa wananchi wote ndani na nje ya mkoa wa Tanga kuhakikisha kuwa siku ya tarehe 14, Februari tunakutana hapa Amboni katika tufurahie mambo mazuri yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ”. Alisema Mhe. Kubecha.
Awali akizungumza katika wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi wa Ngorongoro anayesimamia huduma za utalii na masoko, Mariam Kobelo alisema kwamba kuelekea siku hiyo watatoa fursa kwa wakazi wa Tanga kushiriki kwenye shughuli mbalimbali zitakazo fanyika hapo ili kuendelea kutoa hamasa na kuongeza uwelewa wa shughuli mbalimbali za Uhifadhi zinazofanywa na Mamlaka hiyo.
Alisema shughuli ambayo wanakwenda kuifanya msimu huo wa sikuu ya wapendanao itahusisha mashindano ya Upishi wa vyakula vya asili yatafanyikia amboni pamoja na kutembea ndani ya mapango na kupatiwa elimu juu ya kivutio hiki cha kipekee kilichopo hapa nchini.
Aidha, Kobelo alieleza kuwa ili kuhakikisha siku hiyo itakuwa nzuri na kuwezesha watanzania wengi kushiriki, Mamlaka imeshirikiana na Kampuni ya Utalii ya Smiles Safaris ambayo itatoa huduma za kuwaleta watalii kwenye mapango hayo kutoka mikoa ya Dar es salaam, Arusha, Kilimanjaro na Tanga.
Ambapo alisema gharama za ushiriki kwa kila Mkoa zitatolewa na gharama hizo zitahusisha Chakula, Malazi siku moja, viingilio pamoja na picha.
Mapango ya Amboni Tanga yanayosimamiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) tangu mwaka 2019 na yapo umbali wa Km 9 tu kutoka katikati ya Jiji la Tanga.
Mapango hayo yamefanyiwa maboresho mbalimbali ikiwemo ufungaji wa taa maalum kuwezesha mgeni kuona vivutio vilivyopo ndani ya Mapango sambamba na kuboresha njia za mapito katika eneo la ndani ya mapango hayo ambapo kwa sasa eneo hilo linapokea wageni zaidi ya 30,000 kwa mwaka.
Mwisho
EmoticonEmoticon