Na Oscar Assenga, TANGA
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM)
Taifa Rajab Abdurhaman amesema uwekezaji uliofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu
kwenye sekta ya elimu mkoani Tanga umesaidia kuwaokoa watoto kufanyishwa kazi
za ndani.
Rajabu ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga
aliyasema hayo juzi wakati akizindua maadhimisho ya miaka 48 ya kuzaliwa chama
hicho katika mkutano ulikuwa na lengo la kuunga mkono maamuzi ya mkutano mkuu
maalumu wa CCM.
Maamuzi ya Mkutano Mkuu huo maalumu uliompitisha Dkt
Samia Suluhu kuwa mgombea Urais, Dkt Emanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza pamoja
na kumpitisha Stephen Wasira kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa uliofanyika kwenye eneo la Makorora Jijini Tanga.
Alisema hilo limetokana na uwekezaji wake kupitia
elimu bure ambapo kwa mkoa wa Tanga kila mwezi kwa ada za watoto Rais anatoa Bilioni 1.3 kwa mwezi ambayo ni
bilioni 15.8 kwa miaka.
“Kwa maana ya kipindi cha miaka mitano amewalipua
watoto wetu bilioni 78,Rais asingelipa fedha hizo kwa ajili ya ada za watoto
wetu kwa shule za msingi na sekondari ilipaswa kila mwanafunzi kulipiwa na
mzazi “Alisema
Aidha alisema kutokana na kulipiwa ada za watoto maana
yake amewasaidia baadhi ya majukumu kwenye familia ambazo zisingeweza kulia ada
hiyo ndio sababu zilizopelekea mkutano mkuu kumpitisha kuwa mgombea urais 2025.
“Lakini niwaambie hapa kwamba CCM kupitia ilani Serikali
kwenye suala la elimu ya msingi na sekondari imefanya kazi kubwa sana kwa
kufanya uwekezaji mkubwa hivyo kuongeza ufaulu kwa darasa la saba, kidato cha
nne na cha sita “Alisema
“Hivyo mtu anapohitaji msichana wa kazi na mvulani
wa kazi utasakia nenda korogwe na Lushoto kwa sababu ya watoto wengi kufeli
kutokana na kutokuwa na uwekezaji mkubwa kwenye elimu hivyo kutokana na
uwekezaji wa Rais umesaidia kukua kwa elimu kupandisha ufaulu”Alisema
Aliongeza kwamba leo hii katika matokeo ya darasa la
saba wasiofaulu ni wachache sana na wanakwenda kwenye vyuo vya ufundi na ndio maana
kuwapata wasichana wa kazi au vijana huwezi kuwapata kwa sababu watoto wote
wapo shuleni.
Hata hivyo Mwenyekiti huyo alisema kwamba wanaunga
mkono azimio la mkutano mkuu wa CCM Taifa ambalo lilimpitisha Dkt Samia Suluhu
kuwa mgombea Urais katika uchaguzi Mkuu mwaka 2025.
Alisema pia wanaunga mkono maamuzi kumpitisha Dkt
Emanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza na Dkt Mwinyi kuwa mgombea Urais wa
Zanzibar na wana Tanga wanaupongeza mkutano mkuu kwa kumchagua Stephen Wasira
kuwa makamu CCM Taifa.
“Wapo wanaojiuliza kwanini mkutano Mkuu Mkuu Maalumu
CCM umeamua kwa kura zote za wajumbe kumpitisha Dkt Samia Suluhu nimewahi
kusema mara kadhaa tunapohitaji maendeleo ya kweli kwenye nchi na Taifa lipige
hatua mbele za kimaendeleo jambo la kwanza unalohitaji ni amani.
“Niliwahi kuwaambia Tanga neno amani tunapenda
kulidharau kwa sababu tumezoea kulitamka kila wakati unajua hata chakula
unapokuwa unakula kila siku unafika wakati unakinai ... watanzania neno hilo linahubiriwa
misitiki na kanisani kila wakati inawezekana lakini tujifunze yaliyotokea na
yanayotokea kwenye mataifa ya wenzetu barani Afrika na maeneo mengine duniani
hvyo tuitunze amani yetu”Alisema
EmoticonEmoticon