Makamu
Mwenyekiti wa Taasisi ya Ushauri wa Uhandisi katika miundombinu ya
ujenzi, usarifu wa Miji, Majengo ya Kisasa pamoja na Vituo vya Kimataifa
vya Biashara { ECG } ya Nchini Misri Mhandisi Amri Alouba akimuonyesha
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar michoro iliyotengenezwa na
Wataalamu wa ECG ya jinsi linavyoweza kujengwa eneo la Darajani na kuwa
katika mazingira ya Biashara ya Kimataifa.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na
Wafanyabiashara pamoja na wataalamu wa ushauri wa Uhandisi kutoka Nchini
Misri waliopo Tanzania kuangalia maeneo ambayo wanaweza kuwekeza miradi
ya Kiuchumi.
Meneja
wa Biashara wa Kampuni ya Kimataifa ya AIKAN ya Nchini Misri Bwana
Mohammed Alef Sherief wa kwanza kutoka kushoto akimfahamisha Balozi
Seif hayupo pichani fursa zinazotolewa na Taasisi yake katika kuwajengea
Vijana uwezo wa kufanya Biashara.
Balozi
Seif katika Picha ya pamoja na Wafanyabiashara na wataalamu wa ushauri
wa Uhandisi kutoka Nchini Misri mara baada ya kufanya mazungumzo nao
Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Kushoto ya Balozi Seif ni Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Ushauri wa
Uhandisi katika miundombinu ya ujenzi, usarifu wa Miji, Majengo ya
Kisasa pamoja na Vituo vya Kimataifa vya Biashara { ECG } ya Nchini
Misri Mhandisi Amri Alouba na Balozi wa Tanzania Nchini Misri Balozi
Mohammed Hamza.
Kulia ya Balozi Seif ni Mtaalamu wa Taasisi ya Ushauri wa Uhandisi
katika miundombinu ya ujenzi, usarifu wa Miji ya ECG Mhandisi Sherif
Meurad pamoja na Meneja wa Biashara wa Kampuni ya Kimataifa ya AIKAN ya
Nchini Misri Bwana Mohammed Alef Sherief.
Balozi
Mdogo wa Oman aliyepo Zanzibar Bwana Ali akisalimiana na Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kabla ya kufanya mazungumzo
yao ya Ushirikiano wa kuimarisha uhusiano wa Kihistoria wa muda mrefu
wa kidugu uliopo baina ya Oman na Zanzibar.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na Balozi Mdogo wa
Oman aliyepo Zanzibar Bwana Ali Abdullah Ofisini kwake Mtaa wa Vuga
Mjini Zanzibar.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Taasisi
ya Ushauri wa Uhandisi katika miundombinu ya ujenzi, usarifu wa Miji,
Majengo ya Kisasa pamoja na Vituo vya Kimataifa vya Biashara { ECG } ya
Nchini Misri imeamua kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
katika azma yake ya kusaidia Uchumi wa Zanzibar na ustawi wa Wananchi
wake.
Kiongozi
wa Ujumbe wa Wafanyabiashara wa Misri wanaotembelea Tanzania kuangalia
maeneo wanayoweza kushirikiana na Serikali katika uwekezaji Mhandisi Amr
Allouba alisema hayo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisi kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Mhandisi
Amri Allouba ambae pia ni Makamu Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya
uhandisi ya { ECG } alisema Wataalamu wa Taasisi hizo wako tayari
kuelekeza nguvu zao ndani ya ukanda wa Afrika ya Mashariki, Zanzibar
ikiwa miongoni mwake kutokana na mazingira mazuri ya rasilmali pamoja na
uwekezaji.
Makamu
Mwenyekiti huyo wa Taasisi ya Uhandisi ya ECG alisema Wataalamu wa
Taasisi hiyo tayari wameshaandaa michoro ya jinsi linavyoweza kujengwa
eneo la Darajani na kubadilishwa kuwa katika mazingira ya kisasa ya
Biashara ya Kimataifa.
Mhandisi
Amr alifahamisha kwamba eneo hilo la Darajani upande wa iliyokuwa kituo
cha Dala dala pamoja na Makontena linaweza kujengwa Vituo vya Biashara
bila ya kuathiri mipango Miji iliyowekwa katika Mji Mkongwe wa Zanzibar
ambao umo katika urithi wa Kimataifa.
Wakati
huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
alikutana na Balozi Mdogo wa Oman aliyepo Zanzibar Bwana Ali Abdulla
Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Katika
mazungumzo yao Balozi Seif kupitia Balozi Mdogo huyo wa Oman
aliishukuru Serikali ya Nchi hiyo kwa jitihada inazochukuwa katika
kusaidia harakati za Maendeleo ya Wananchi wa Zanzibar.
Mapema
Balozi Mdogo wa Oman aliyepo Zanzibar Bwana Ali Abdulla alimuhakikishia
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Nchi yake itaendelea kuiunga
mkono Zanzibar katika harakati zake za kuelekea kwenye maendeleo.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
1/8/2015.
EmoticonEmoticon