Mtangaza
nia ya kuwania nafasi ya Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA), Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa
akiwapungia maelfu ya wafuasi na wapenzi wa Chama hicho, wakati
alipowasili kwenye Ofisi ya Makao Makuu ya Chama hicho, Kinondoni Jijini
Dar es Salaam jioni ya leo. Mh. Lowassa alifika ofisini hapo kurudisha
fomu za kuomba ridhaa ya Chama hicho, kuwania Urais kwenye Uchaguzi Mkuu
unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.Kulia kwake ni Mbunge wa
Jimbo la Arumeru Magharibi, Mh. Godluck Ole Medeye alieambatana nae.
Mtangaza
nia ya kuwania nafasi ya Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA), Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa
akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA - Zanzibar, Salum Mwalim
wakati akilakiwa kwenye Makao Makuu ya Chama hicho, Kinondoni Jijini Dar
es salaam leo.
Mtangaza
nia ya kuwania nafasi ya Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA), Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa
akiwasalimia wafuasi wa Chama hiyo kwa ishara ya vidole viwili.
Sehemu ya Viongozi wa CHADEMA waliokuwepo kwenye hafla hiyo.
Baadhi ya Wadau walioambatana na Mh. Lowassa.
Wakitambulishwa.
Mkurugeni
wa Oganaizesheni na Uratibu wa Kanda wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA), Benson Kigaila akionyesha fomu zenye idadi ya
wananchi waliomdhani Mtangaza nia ya kuwania nafasi ya Urais wa Tanzania
kupitia Chama hicho, Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa. ambapo
jumla ya wananchi 1,662,397 walijitokea katika maeneo mbali mbali
kumdhamini Mgombea huyo.
Mtangaza
nia ya kuwania nafasi ya Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA), Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa (wa
pili kulia) akikabidhi fomu hizo kwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Prof.
Abdalaah Safari wakati wa hafla fupi ya kurudisha fomu hizo,
iliyofanyika jioni ya leo kwenye Ofisi za Makao Makuu ya CHADEMA,
Kinondoni Jijini Dar es salaam. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa
Wadhamini wa CHADEMA, Mh. Arcado Ntagazwa na kulia ni Naibu Katibu Mkuu
wa CHADEMA - Zanzibar, Salum Mwalim.
Mtangaza
nia ya kuwania nafasi ya Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA), Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa (kulia)
na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Prof. Abdalaah Safari wakionyesha fomu
hizo kwa wanahabari.Kushoto ni Mwenyekiti wa Wadhamini wa CHADEMA, Mh.
Arcado Ntagazwa.
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Prof. Abdalaah Safari akizipitia fomu hizo.
Mwanasheria wa CHADEMA, Mh. Mabere Marando akizipitia fomu hizo kama zimejazwa sawa sawa.
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Prof. Abdalaah Safari akizungumza machache baada ya kupokea fomu hizo.
Makamu
Mwenyekiti wa CHADEMA, Prof. Abdalaah Safari akipongezwa na Mtangaza
nia ya kuwania nafasi ya Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA), Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa.
Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA - Zanzibar, Salum Mwalim akizungumza.
Sehemu ya Wabunge wa CHADEMA waliokuwepo.
EmoticonEmoticon