 |
Balozi Dr Mahiga -Iringa mjini.
Na matukiodaimaBlog
ALIYEKUWA
balozi wa kudumu wa umoja wa mataifa (UN) na mgombea urais katika
mchakato wa ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) balozi Dr Augustono
Mahiga anayeomba kuteuliwa kuwa mgombea ubunge jimbo la Iringa mjini
kupitia CCM amewashangaa makada maarufu wa chama hicho walioshindwa
katika mchakato wa ndani ya chama kwa nafasi ya urais kuhama chama hicho
kuwa hao hawakuwa na mapenzi ya kuwatumikia watanzania na kuwa
watazunguka kote ila chama makini ni CCM pekee na kuwataka wana CCM
jimbo la Iringa mjini kumpa nafasi yeye ili kuondoa masalia ya Chadema .
Balozi
Dr Mahiga alisema kuwa wana CCM hao walioanza kuhama chama kwa
kukosa nafasi ya urais hawakuwa na mapenzi mema na CCM bali walikuwa
wawametanguliza maslahi yao mbele na kuacha kuangalia maslahi ya Taifa
na chama hivyo ni vema watanzania kuwatazama kwa jicho la tatu na
ikiwezekana kuwachunguza japo kwa miaka 5 bila kuwachagua kuwa
viongozi wao.
Alisema
kuwa kama suala ni uongozi kwa ajili ya kuwatumikia wananchi na
chama kulikuwa hakuna sababu ya kuhama chama ama kuanza kutukana chama
kwa sasa ila wangeweza kushuka chini na kugombea nafasi za chini
ukiwemo udiwani ama ubunge kama ambavyo yeye alivyoshuka na kugombea
ubunge ili kuwatumikia watanzania kwa ngazi ya ubunge.
"Kila
nafasi ndani ya chama ina maana kubwa katika kutumikia watu hivyo
kuhama chama si jambo jema na upande wa vyama lazima kuwa makini na
wanachama wanaohama vyama kwa sasa ili kupata nafasi za uongozi iwapo
watakosa nafasi hizo bila shaka watachukua hatua ya kuvuruga nguvu ya
vyama hivyo ama kuhama vyama "
Balozi
Dr Mahiga aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari
mjini Iringa kuhusiana na mchakato mzima wa kumpata mgombea Urais wa CCM
Dr John Magufuli na mchakato wa kura za maoni katika ngazi ya
udiwani na ubunge katika jimbo la Iringa mjini ambako ni mmoja kati
ya wana CCM 14 wanaoomba kuteuliwa kuwa wagombea wa ubunge .
Alisema
akiwa kati ya wana CCM 41 waliojitokeza kuchukua fomu ya Urais hana
kinyongo na uteuzi wa mgombea Urais wa CCM Dr Magufuli kwani ni mtu
makini na safi ambae viatu vya Rais wa awamu ya nne Dr Jakaya Kikwete
ataweza kuvimudu vema kutokana na kutokuwa mtu wa kulipisha kisasi
na hana makuu na mtu zaidi ya kulitumikia Taifa .
Hivyo
alisema iwapo wana CCM jimbo la Iringa mji watamchagua yeye kuwa
mgombea ubunge jimbo hilo wawe imani ya kulikomboa jimbo hilo
asubuhi saa 12 kutoka kwa Chadema chini ya aliyekuwa mbunge wa jimbo
hilo mchungaji Peter Msigwa kwani alisema si kweli kama Chadema Iringa
mjini wananguvu kubwa kuliko ya CCM na ukitazama idadi ya wenyeviti wa
mitaa ambao CCM inao wenyeviti 104 huwezi linganisha na wale 64 wa
Chadema kabla ya wenyeviti wake 13 kuvuliwa nafasi zao na mahakama.
Alisema
dawa ya ushindi wa kishindo kwa CCM Iringa mjini ni moja pekee
kuvunja makundi na kuwa kundi moja la ushindi baada ya zoezi la kura za
maoni kumalizika .
|
 |
Dc Mwamoto kulia akiwa na mbunge wa Kalenga Godfrey Mgimwa ,mwamoto ni mgombea ubunge Kililo
Mkuu
wa wilaya ya Kaliuwa mkoani Tabora Bw Venance Mwamoto ambae anawania
kuteuliwa kuwa mgombea ubunge jimbo la Kilolo mkoani Iringa amesema
kuwa tishio la kutaka kuuwawa kwake majuzi baada ya kufyatuliwa
risasi katika gari lake wakati akitoka katika kampeni kata ya Ilula
bado haimtishi katika safari yake ya kuwatumikia wananchi wa jimbo
la Kilolo linaloongozwa na Prof. Peter Msolla .
Kwani
alisema moja kati ya ahadi yake kubwa kwa wananchi wa Kilolo ni kuona
amawatumikia kwa kasi zaidi na kumaliza kero ya maji katika mji wa
Ilula na changamoto nyingine ambazo hazijapatiwa ufumbuzi kwa kipindi
kilichopita na mbunge aliyekuwepo .
Mwamoto
alisema kuwa kazi nzuri aliyoifanya kwa nafasi ya ukuu wa wilaya
kwa kipindi kifupi ambacho Rais Dr Jakaya kikwete alipomteua kwa kuwa
mkuu wa wilaya ya Kibonde na Kaliuwa ni wazi ni kipimo tosha na
heshima kubwa ya wananchi wa Kilolo kujivunia na wategemee makubwa
zaidi iwapo watamchagua kuwa mbunge wao kwa sasa .
|

waziri Lukuvi - Isimani
Mbunge
wa jimbo la Isimani Bw Wiliam Lukuvi amewaomba wananchi wa jimbo
hilo hasa wanachama wa CCM kuendelea kujenga imani kwake na kuwa ndani
ya CCM kuna Demokrasi na kila mwanachama ana sifa ya kugombea nafasi
yoyote ndani ya chama japo kipimo cha kuchaguliwa bado kipo kwa
wananchi wenyewe ambao wanaweza kumpima kwa kazi alizofanya badala ya
kushawishiwa kwa manenio bila vitendo.
Lukuvi
ambae ni waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amesema kama si
wana Isimani kuonyesha ushirikiano wao kwake na hata kumchagua katika
nafasi hiyo ya ubunge basi heshima ambayo ambayo wana Iringa
wameipata kupitia wizara yake leo isingekuwepo .
Alisema
suala la migogoro ya ardhi amepata kulishughulikia kwa umaniki
mkubwa na kuwa sulaa hilo pia lilikuwa ni kero kubwa hata kwa wananchi
wake wa jimbo la Isimani ila kwa sasa kwa kiasi limeanza kupungua na
kuwa iwapo wataonyesha imani yao tena wategemee kuona maendeleo makubwa
zaidi katika jimbo hilo na kutaka baadhi ya kazi kubwa ambazo
zimefanyika kuwa ni pamoja na barabara ya lami ya Iringa- Dodoma, umeme
vijini , ujenzi wa shule pamoja na ujenzi wa nyumba bora kwa kupata
bati za ruzuku .
"Tumekuwa
pamoja muda wote katika maendeleo na matatizo hivyo lazima kila
safari ina wasindikizaji wake na siku zote penye maendeleo ndipo
panapopendwa na wengi ila bado kwa tathimini yetu Ismani ya leo sio
ya jana . nimekomesha ulanguzi wa mazao kama mpunga ,alizeti kwa
kufunga mashine"
Godfrey Mgimwa -Kalenga
Mbunge
wa jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa anayeomba kuteuliwa tena kuwa
mgombea wa CCM nafasi ya ubunge amewashukuru wananchi wa kalenga kwa
kuonyesha ushirikiano kwake na kuwa hadi sasa amepata kutekeleza ahadi
zake kwa wananchi kwa asilimia 99 na kuwa zipo changamoto mbali mbali
ambazo watampa tena nafasi ya ubunge atakwenda kuzifanyia kazi .
Mgimwa
ambae amepata kuongoza jimbo hilo kwa mwaka mmoja pekee akichukua
nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Dr Wiliam
Mgimwa aliyefariki duni mwaka jana mwanzioni ,alisema zilikuwepo ahadi
mbali mbali ambazo ziliachwa na mbunge aliyepita na tayari zote
amezikamilisha kwa kipindi cha mwaka mmoja na kubwa anajivunia kuanzisha
vikundi vya Vicoba zaidi ya 60 ,ujenzi wa barabara , maji vijiji
,umeme na uchangiaji wa ujenzi wa zahanati ,shule na maabara na kuwa
zaidi ya Tsh milioni 100 amepata kutumia kwa kuchangia miradi ya
maendeleo jimboni.
Share this
EmoticonEmoticon