JESHI la Polisi Mkoa wa Tanga linaendelea na uchunguzi wa tukio la Bondia Hassan Mwakinyo (29) kwa tuhuma za kumjeruhi na kumshambulia mkazi wa Sahare Jijini Tanga Mussa Ally (21) mvuvi mkazi wa Sahare Jijini Tanga.
Akizungumza leo na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Almachius Muchunguzi alisema kwamba baada ya tukio hilo wameanza uchunguzi huku wakiendelea kumshikilia.
Kamanda Muchunguzi alisema kwamba katika tukio hilo lilitokea Machi 4 mwaka huu nyumbani kwa Hassani Mwakinyo ambapo baada ya uchunguzi wa tukio hilo kukamilika watamfikisha mahakamani.
“Mara baada ya uchunguzi wa shauri hili kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria “Alisema
Aidha alisema Jeshi hilo linaendelea kutoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu sambamba na kuacha kujihusisha na vitendo viovu hasa matukio ya kujichukulia sheria mikononi kwa kufanya hivyo ni kosa la jinai.
Kwa mujibu wa Kamanda Muchunguzi alisema Mwakinyo baada ya kuhojiwa alieleza kwamba huyo mtu alimchukulia kama mwizi lakini kumchulia mtu kama hivyo haimpi mtu mamlaka ya kumchukulia sheria mkononi ndio maana Jeshi la Polisi linamshikilia kuendelea kuchunguzi kujua kiini cha kumshambulia mhanga huyo.
“Lakini kumekuwepo kwa tuhuma mbalimbali zinazomtuhumu Mwakinyo kufanya vitendo kama hivyo miaka ya nyuma na hivyo kama kuna mtu yoyote anataarifa Jeshi la Polisi wanaendelea kufanya uchunguzi kama mtu anataarifa hizo za nyuma azilete zitazifanyia kazi”Alisema RPC.
Mwisho
EmoticonEmoticon