IMEWAKWA DESEMBA 17 Na Dege Masoli, Korogwe.
Baadhi ya viongzi wa madhehebu mbalimbali ya dini Wilayani hapa, wamekiri kuwa ukosefu wa elimu ya ushauri nasaha kuhusu VVU na Ukimwi na jinsi ya kuwahudumia waathirika wa ungonjwa huo iliwafanya kuwa kikwazo katika mapambano ya unyanyapaa.
Viongozi
hao walieleza hayo wakati wa mafunzo ya jinsi ya kushughulikia
unyanyapaa,madhara na faida za kutokuwepo kwa unyanyapaa yaliyoambatana
na kupima afya zao kwa hiari, walidai kuwa kukosa elimu hiyo ili kuliwafanya wawe kikwazo bila ya wao kujijua.
Katika mafunzo hayo ya siku mbili viongozi 30 wa madhehebu ya dini kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Korogwe walipima afya zao kwa hiari ambapo mtaalamu wa upimaji afya, Joice Mwanga alisema kuwa maambukizi yalikuwa asilimia 0% ya washiriki wote.
Wakizungumza na Blog hii, Viongozi hao walieleza kuwa zoezi la upimaji wa afya limefanikiwa kutokana na elimu waliyoipata kuwapa mwanga
wa kujitambua tofauti na walivyokuwa awali ambapo suala la kupima afya
lilikuwa ni kinyume na imani na taratibu za dini zao.
“Tumejifunza mengi lakini kubwa ni kutambua jinsi ya kushughulikia unyanyapaa ndani ya jamii, madhara na faida za kutokuwepo kwa unyanyapaa huo……. huu ni mwanga kwetu” alisema Yahaya Yussuph.
Naye Richard David yeye alieleza kuwa .inawezekana wao walikuwa kikwazo cha kupunguza kama siyo kuondoa kabisa tatizo hilo bila ya wao kujua na kwamba sasa wataendeleza mapambano ya unyanyapaa na upimaji afya kwa hiari huku wakiwa mfano kwa wengine.
Janeth Mshana alibainisha
kuwa ukosefu wa elimu ya unyanyapaa na faida za upimaji wa afya
lilikuwa tatizo si kwa waumini pekee lakini pia hata kwa viongozi wa
dini lilikuwa ni jambo la miujiza ambalo halikuwa rahisi kulitangaza
bayana mbele ya jamii zaidi ya kuegemea katika masuala ya kiimani pekee.
Omari Abdalah alisema
kuwa tatizo hilo lilikuwa kikwazo katika mapambano ya harakati za
unyanyapaa na kupima afya na kwamba baada ya kupata mafunzo hayo
watahakikisha mabadiliko ndani ya nyumba za ibada na jamii kwa ujumla
katika maeneo yao yanapatikana.
Walisema kuwa wamepata nguvu na muamko mpya kwani awali walikuwa hawana uwezo wa kujieleza juu ya suala zima la VVU na ukimwi mbele ya waumini wao jambo walilodai kuwa sasa si kujieleza pekee bali na hata kutoa maelezo kwa mtu mwingine, kumuandaa mtu na majibu yake yawe ya ugonjwa ama uzima na jinsi ya kukabiliana na matatizo
aliyonayo.
Alisenma
kabla ya mafunzo hayo viongozi wengi wa dini walikuwa na mtazamo
tofauti juu ya maambukizi ya VVU na ukimwi na kwamba ilikuwa vigumu
kumkabili mtu kutokana na ukweli kuwa uathirika lilionekana ni tendo la aibu na linaloashiria kifo.
Mratibu wa Mtandao wa Viongozi wa dini wanaoishi kwa matumaini nchini, Tanzania Network of Religious Leaderrs Living with or Personally Aftected by HIV (TANERELA ) , Mchungaji Amin Sandewa alisema kuwa mafunzo hayo yamefanyika baada ya kuonekana kuwepo kwa tatizo la
kiuelewa na kulieleza suala zima la HIV kwa viongozi hao..
Sendewa alieleza kuwa mtandao umetoa elimu hiyo kwa viongozi wapatao 30 kati ya waliyopangwa kupata elimu hiyo katika Wilaya ya Korogwe na kwamba huo ni mpango mkakati wa Mtandao huo wa kuwawezesha viongozi kuwa mabalozi wazuri wa mapambano zidi ya ukimwi na kupima unaondelea nchini nzima.
EmoticonEmoticon