OFISI YA TAIFA YA UKAGUZI (NAOT) YAWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WA HABARI MKOA WA TANGA

December 18, 2025


Na Oscar Assenga, TANGA.

OFISI ya Taifa ya Mkaguzi (NAOT) imeendesha mafunzo yanayolenga kuwajengea uwezo waandishi wa habari mkoa wa Tanga na mikoa mengine kuhusu masuala yanayohusiana na ripoti za Ukaguzi zinazoandaliwa na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo hayo ya siku moja, Mkuu wa Kitengo cha Mawasilian Serikalini Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) Focus Mauki alisema wanafanya mafunzo hayo ambayo kwa mujibu wa mpango mkakati wa ofisi ya Taifa ya Ukaguzi unao wataka wawe na mahusiano ya karibu na wadau wanaoafanya nao kazi.

Alisema kwamba wadau hao ni pamoja na vyombo vya habari na asasi za kiraia na Bunge pamoja wafadhili na wengineo ambao wanaguswa na ripoti za ukaguzi wa mdhibiti mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wanaandaa mafunzo kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu masuala ya ukaguzi.

“Leo Desemba 17,2025 tumekuja kutoa elimu kwenye eneo lingine la Ukagzi wa Serikali za Mitaa kwa hiyo leo waandishi wa habari wa Tanga Press Club tutajifunza kuhusu masuala la utendaji kazi wa ofisi,sheria zinazotuongoza,majukumu ya CAG ni yapi na aina ya hatia za ukaguzi na ripoti za ukaguzi ambazo CAG anazitoa”Alisema Mauki .

Alisema katika mafunzo hayo wanahabari hao watapitishwa kwenye mada mahususi wanaye mtaalamu ambaye atawapitisha kwenye mada mahususi na wanaye mtaalamu kutoka Divisheni za Serikali za Mitaa .

Alieleza kwamba watawapitisha kuhusu ukaguzi wa Serikali za mitaa,mafunzo hayo yanandaliwa na CAG yanahusisha pia asasi za kiraia na watakapotoa Tanga wanaenda Pwani na Morogoro huku akieleza kwamba mafunzo hayo ni endelevu kwa kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali.

Mauki alisema kwamba hivyo baada ya mafunzo hayo wanamatumainia kupata mrejesho kwa waandishi wa habari Tanga kutokana na kwamba wao wanashiriki kwenye masuala la maendeleo kwenye mkoa wa Tanga.

“Hivyo tunaamini waandishi wa habari pia ni wadau ambao wanaweza kutupa mrejesho wa matokeo ya ripoti za mkaguzi wa CAG na mapendekezo ya utekelezaji wa ripoti hizo na kupendekeza maeneo ambayo ni muhimu CAG tunaweza kuyafanyia kazi na kuweza kuleta tija kwa serikali yetu”Alisema .

Hata hivyo alisema kwamba ofisi hiyo imeendelea kupata ushirikiano kutoka kwa wadau mbalimbali ikiwemo Bunge na Serikali na ndio maana serikali imekuwa na utashi wa kupokea ripoti na kuipeleka Bungeni ili kuweza kujadiliwa na kamati ya bunge kuwaita maafisa masuhuli kwa ajili ya kujadiliana nao kuhusu mapendekezo yanayotolewa na CAG.

Alisema kwamba wanapotoa mafunzo hayo wanatarajia kupata mrejesho huku akieleza kwamba ofisi hiyo ina mfumo maalumu ambao mwananchi anaweza kuutumia kupeleka taarifa yoyote ambayo ameiona ili kuweza kuwafikia.

Mauki alisema hata wanahabari wanaweza kuingia kwenye tovuti hiyo ili kupelekea taarifa CAG ziweze kufanyiwa huku akieleza kwamba wanapokutana na waandishi kwenye majukwaa kama hayo wanapata fursa ya kuwaeleza majukumu yao na wao kuwaeleza walioanyo,

Awali akizungumza Mkaguzi Mkuu wa Nje Mkoa wa Tanga Hamu Mwakasola alisema kwamba mpango mkakati wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi inatambua kwamba mpango huo unatambua vyombo vya habari ni kiungo muhimu katika taarifa za ukaguzi na wananchi.


Alisema kwamba kwa kuwa wao ndio wanaobeba jukumu la kuifafanuzi na kuchambua kwa kuifikisha taarifa hiyo kwa umma kwa lugha rahisi inayoeleka.

Alisema kupitia mkakati huo wamejipanga kuendelela kuboresha uwazi katika utoaji taarifa za ukaguzi ili kuimarisha mawasiliano na wadau kwa kuwajengea uelewa mpana kuhusu kazi,majukumu na mipaka ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.

Alisisitiza kwamba mafunzo hayo ni ushahidi wa dhamira hiyo ya kuweza kuongeza uwezo wa waandishi wa habari katika kusoma ,kuchambua na kuripoti kwa usahihi ripoti za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali.

Naye kwa upande wake Katibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Tanga (TPC) Mbonea Herman alishukuru ofisi ya CAG na kueleza kwamba yamefika wakati muafaka na watakwenda kuandika habari za ukaguzi kwenye misingi ambayo inakuwa inawadhirisha wananchi.

Alisema kwamba kutokana na mafunzo hayo alisema wapo kwenye mpango mkakati wa kuhakikisha waandishi wa habari wanakuwa na uelewa mpana wa masuala mbalimbali na kuisaidia jamii katika masuala ya fedha.

Mwisho.


Share this

Related Posts

Previous
Next Post »