Na Masanja Mabula ,Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa
Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, ametembelea uwanja wa Amaan
Mjini Zanzibar kukagua maendeleo ya zoezi la uwekaji wa nyasi bandia katika
uwanja huo.
Meneja wa uwanja huo
Khamis Ali Mzee, amesema zoezi hilo linaendelea vizuri, huku wakiendelea
kukusanya vifaa zaidi kwa ajili ya kukamilisha zoezi hilo kwa wakati muafaka.
Amesema vifaa
vinavyoendelea kukusanywa kwa sasa ni pamoja na mchanga maalum ambao unakwenda
sambamba na uwekaji wa nyasi hizo ili kuweka umadhubuti zaidi wa uwanja huo.
Kwa upande wake
mkandarasi wa uwekaji wa nyasi hizo bw. Ben Mushi kutoka kampuni ya EKIKA ya
Dar es Salaam, amesema mvua zinazoendelea kunyesha zinazorotesha zoezi hilo.
Hata hivyo amesema watafanya kila juhudi kuona kuwa zoezi hilo linakamilika kwa wakati, ili uwanja huo uweze kutumika kwa sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi, zinazotarajiwa kufika kilele chake tarehe 12 Januari, 2014. |
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon