Kaimu Meneja Mgodi wa Barrick Bulyanhulu Leon Ebondo akizungumza wakati Barrick Bulyanhulu Family Day
**
Mgodi wa dhahabu wa Barrick Bulyanhulu uliopo katika halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga umeandaa tukio la Family Day 2025, ambalo limekutanisha mamia ya wanafamilia wa wafanyakazi wa Mgodi huo ,viongozi wa Serikali na vijiji vinavyozunguka mgodi na wakazi wa eneo hilo ambapo wameungana na kufurahi pamoja.
Tukio hilo ambalo hufanyika kila mwaka mwishoni mwa mwezi Desemba lilipambwa na maonesho ya shughuli zinazofanyika katika mgodi huo, michezo mbalimbali ya watu wazima na watoto, chakula cha pamoja, vinywaji , muziki na kubadilishana mawazo.
Kaimu Meneja Mgodi wa Barrick Bulyanhulu Leon Ebondo ,amewakakaribisha na kuwashukuru wote waliohudhuria hafla hiyo ambayo imewezesha wanafamilia za wafanyakazi kuona kazi zinazofanywa na mgodi sambamba na kudumisha mshikamano na jamii inayozunguka mgodi huo.
EmoticonEmoticon