MUONEKANO WA MAJENGO YA KAMPASI YA LINDI YA UDSM AMBAYO WAZIRI MKUU DKT MWIGULU ALIWEKA JIWE LA MSINGI JUMAMOSI DISEMBA 20, 2025

December 22, 2025




Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Kampasi ya Lindi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), katika hafla iliyofanyika eneo la Ngongo, Manispaa ya Lindi.

Ujenzi wa kampasi hiyo, ambayo majengo yake ni hayo pichani, unatekelezwa kwa mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), ukiwa na lengo la kusogeza elimu ya juu karibu na wananchi na kuimarisha mchango wa elimu katika maendeleo ya taifa.

Kwa mujibu wa UDSM, bajeti ya mradi ni Shilingi bilioni 14.8, ikihusisha ujenzi wa jengo la utawala na taaluma lenye madarasa sita yatakayohudumia wanafunzi 360, karakana ya kilimo, maabara yenye uwezo wa wanafunzi 125, mabweni mawili kwa wanafunzi 200, pamoja na Kituo cha Utafiti cha Ruangwa chenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 50.

Mradi huo unatekelezwa na Mkandarasi Shandong Hi-Speed Dejian Group Ltd chini ya usimamizi wa Geometry Consultants Limited, ambapo utekelezaji umefikia asilimia 60.

Kampasi ya Lindi inatarajiwa kutoa programu za uzamili, shahada, stashahada na vyeti, hususan katika sekta za kilimo, ufugaji, ufugaji wa nyuki na teknolojia ya chakula, na kuchochea ajira, tafiti bunifu na maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika Ukanda wa Kusini.







Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »