TIMU 43 KUSHIRIKI UMISETA NGAZI YA WILAYA YA TANGA.

March 20, 2013
Na Mwandishi Wetu,Tanga.
JUMLA ya timu 43 zinatarajiwa kushiriki mashindano ya Umoja wa michezo shule za Sekondari nchini (Umiseta) ngazi wilaya ya Tanga ambayo yanatarajiwa kuanza Machi 22 mwaka huu.
 
Mratibu wa Mashindano hayo, Damiani Mabena aliiambia blogi hii kuwa mashindano hayo yatachezwa viwanja saba ambavyo zimeteuliwa na kamati ya inayoratibu mashindano hayo.
Mabena alisema vituo vitakavyochezewa ni shule za sekondari Popatlaly, Usagara, Galanosi,Rosimini, Kiomoni, Tanga Ufundi pamoja na kituo maalumu kilichopo Ndaoya na Marungu
 
Aliitaja michezo ambayo itashindaniwa katika mashindano hayo msimu huu kuwa ni mchezo wa mpira wa miguu,mchezo wa mpira wa wavu,mchezo wa riadhaa,mchezo wa kikapu,mchezo wa mpira wa mikono,mpira wa meza na mpira wa pete.
Mratibu huyo alizitaka shule ambazo zimethibitisha kushiriki kuwa ni Pande,Kirare,Pongwe, Marungu,Mwapachu, Chumbageni, Mnyanjani,Mikanjuni,Kihere,Toledo,Macechu,Nguvumali,Old Tanga, Haki, Besha, Japani,Eckernforde Girls, Rosmini, Horten, Chongoleani, Mabokweni, Tongoni,Maweni,Maawal na Arafah.
Alizitaja shule nyingine kuwa ni Eckernforde, Popatlaly, Usagara, An –Noor,Al-Kheir,St.Christina,Tanga Ufundi, Kiomoni,Sahare, Jumuiya, Mkwakwani, Galanosi, Eckernforde Cambridge, Ndaoya, Coastal, Elohim, Msambweni na Don Bosco.
 Mabena alizitaka timu za shule zinazotarajiwa kushiriki mashindano hayo zianze maandalizi mapema ili kuweza kuleta msisimuko zaidi wakati wa mashindano hayo.
 
Mwisho.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »