Na Boniface Wambura,Dar es Salaam.
Timu ya Taifa ya
Morocco (Lions of the Atlas) inatarajiwa kuwasili nchini keshokutwa Ijumaa kwa
ndege ya Emirates tayari kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Tanzania
(Taifa Stars) itakayochezwa Jumapili katika Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Msafara wa timu hiyo yenye watu 58 wakiwemo maofisa 19
na waandishi wa habari 12 utawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere (JNIA) saa 8.55 mchana na utafikia hoteli ya Kilimanjaro Hyatt
Regency.
Siku hiyo Morocco inatarajia kufanya mazoezi jioni
kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, na Jumamosi itafanya mazoezi yake ya
mwisho kwenye Uwanja wa Taifa kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa saa 9 kamili
alasiri.
Wachezaji walioko kwenye kikosi hicho chini ya Kocha
Rachid Taoussi ni Nadir Lamyaghri, Anas Zniti, Yassine Bounou, Younnes
Bellakhadar, Abdellatif Noussair, Abderrahim Achchakir, Zoheir Feddal, Younnes
Hammal, Zakarya Bergdich na Abdeljalil Jbira.
Issam El Adou, Kamel Chafni, Salaheddine Saidi, Mohamed
Ali Bamaamar, Abdelaziz Barrada, Salaheddine Aqqal, Abdessamad El Moubarky,
Nordin Amrabat, Chahir Belghazouani, Abdelilah Hafidi, Youssef Kaddioui, Brahim
El Bahri, Hamza Abourazzouk na Youssef El Arabi.
Wakati huo huo, tiketi kwa ajili ya mechi hiyo zitaanza
kuuzwa keshokutwa katika vituo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni
Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha
Mafuta Buguruni, Uwanja wa Taifa na Dar Live Mbagala.
Milango siku ya mechi kwa ajili ya watazamaji
itafunguliwa saa 6 kamili mchana.
Mwisho.
EmoticonEmoticon