HIFADHI YA NGORONGORO YASHIRIKISHA UZINDUZI WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA.

October 07, 2025 Add Comment

Na Mwandishi wetu, Ngorongoro 

Tarehe 7 Oktoba, 2025.

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imewashirikisha baadhi ya watalii katika uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja ambapo wageni hao wameipongeza mamlaka hiyo kwa kuendelea kuboresha huduma na miundo mbinu ya utalii.

Wakizungumza katika hafla iliyofanyika kwenye lango kuu la kuingia Hifadhi ya Ngorongoro eneo la Loduare baadhi ya watalii hao wamesema kuwa wanaridhishwa na huduma zinazotolewa na mamlaka hiyo  na kusema  wataendelea kuwashawishi wageni wengine kutoka nchi zao kutembelea Ngorongoro.

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa uhifadhi anayeshughulikia Huduma za Utalii Mariam Kobelo amewahakikishia wageni hao kuwa mamlaka itaendelea kuboresha huduma zake na kwamba watafanyia kazi kwa ukaribu maoni yote yatakayotolewa na wateja ili kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali za kuongeza wageni katika sekta ya utalii.

“Tunaitumia wiki hii ya huduma kwa wateja kuendelea kupokea maoni mbalimbali ya wateja wetu,tumejipanga vizuri kuhakikisha kuwa tunashughulikia maoni yote yatakayotolewa ili kuunga mkono kwa vitendo juhudi za serikali yetu za kuboresha utalii nchini,”alisema Mariam.

Wiki ya Huduma kwa wateja ni mahsusi kwa ajili ya kutoa nafasi kwa watumishi wa sekta mbalimbali kuwasikiliza wateja wao na kufanyia kazi maoni ya wateja wao.

DKT.SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA WANANCHI WA MISUNGWI MKOANI MWANZA

October 07, 2025 Add Comment

Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa Misungwi katika muendelezo wa muendelezo wa Kampeni za Uchaguzi kwa CCM, mkoani Mwanza tarehe 07 Oktoba, 2025.

Matukio mbalimbali katika mkutano wa hadhara wa Kampeni wa Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan uliofanyika Misungwi mkoani Mwanza tarehe 07 Oktoba, 2025.

Shamra shamra za mapokezi ya Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuwasili Misungwi mkoani Mwanza tarehe 07 Oktoba, 2025.

.

WAZIRI MKUU ATOA MAAGIZO WIZARA YA MADINI

October 07, 2025 Add Comment

-Aitaka ifuatilie kampuni zilizoshika maeneo bila kuyaendeleza

-Aipongeza kampuni ya Huaer International kwa uwekezaji.

-Asisitiza uwekezaji huo ni utekelezaji wa Maono ya Rais Dkt. Samia

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Madini kufanya ufuatiliaji wa makampuni ya madini ambayo yameshilikilia maeneo kwa muda mrefu lakini hawajayaendeleza mpaka sasa yakiwemo makampuni matatu wilayani Ruangwa

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa makampuni ya Nachu, Uranex na Paco Gems Ltd yanapaswa kusema hatma ya maeneo waliyoyahodhi kwa muda mrefu vinginevyo ardhi hiyo itarudishwa kwa wananchi.

Ametoa agizo hilo leo Jumanne (Oktoba 07, 2025) alipotembelea kampuni ya uchimbaji wa madini Huaer International Limited katika kijiji cha Ng’au Ruangwa mkoani Lindi.

“Kampuni ya Paco Gems tangu 2009 mpaka leo hakuna maendeleo, tunatoka Utanex pale Chunyu, wameshalipa fidia tangu 2012 lakini mpaka leo hii hakuna maendeleo yoyote, ipo kampuni ya Nachu ambayo ilipata heshima ya kusaini mkataba mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mpaka leo hii wamepotea na hakuna taarifa.”

Mheshimiwa Majaliwa ameipongeza kampuni ya Huaer International Limited ambayo imefanikiwa kuanza mchakato wa uwekezaji ndani ya kipindi kifupi baada ya kupata vibali vyote muhimu.

“Kampuni yako ambayo imeanza ukaguzi mwaka 2024, ukapata matokeo mwaka huohuo na kuomba vibali mwaka huohuo, leo mmeanza utekelezaji wa ujenzi na mmefikia hatua hii, ninyi mnapaswa kupongezwa na mnapaswa kuwa mfano wa makampuni haya mengine tata.”

Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa ujenzi wa kampuni hiyo ni utekelezaji wa maono ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuzalisha ajira kwa Watanzania kupitia uwekezaji. “Kampuni hii ndiyo inaanza na inaendelea na ujenzi mtakapokamilisha mtatoa nafasi ya Watanzania na Wana-Ruangwa kupata ajira hapa.”

Pia, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa vijana wa Kitanzania waliopata nafasi ya kufanya kazi katika kampuni hiyo kufanya kazi kwa bidii, weledi, nidhamu na uaminifu “Tunahitaji kuwahakikishia hawa wawekezaji kwamba tunaajirika na tunaweza kufanya kazi hizi.

Kwa Upande wake Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala ameishukuru Serikali kwa kuendelea kufungua fursa za uwekezaji kwa mkoa wa Lindi na Tanzania kwa ujumla ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa kichocheo cha maendeleo kwa wakazi wa maeneo hayo.

Amesema kuwa uwekezaji wa kampuni ya Huaer utakuwa ni moja ya fursa kubwa sio tu kwa uchumi wa Wilaya ya Ruangwa au Mkoa wa Lindi bali Tanzania kwa ujumla

“Sisi upande wa Mkoa tunaendelea kuahidi kutekeleza sera zote za uwekezaji ambazo Serikali inaziweka na kuendelea kushirikiana na wawekezaji kwa kuweka mazingira rafiki ili waendelee kuwa kwa wingi katika mkoa wetu”

Thamani ya mradi huo ni dola za marekani milioni 20.

DKT.SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA WANANCHI WA BUHONGWA,NYAMAGANA JIJINI MWANZA

October 07, 2025 Add Comment
Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa Kata ya Buhongwa, katika muendelezo wa Kampeni za Uchaguzi kwa CCM, Nyamagana mkoani Mwanza tarehe 07 Oktoba, 2025.

KATIBU Mkuu wa CCM Dkt Asha Rose Migiro akizungumza katika muendelezo wa Kampeni za Uchaguzi kwa CCM, Nyamagana mkoani Mwanza tarehe 07 Oktoba, 2025.

 Sehemu ya Wananchi wa Kata ya Buhongwa waliohudhuria mkutano wa hadhara wa Kampeni wa Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan mkoani Mwanza tarehe 07 Oktoba, 2025.

Shamra shamra za mapokezi ya Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuwasili Buhongwa mkoani Mwanza tarehe 07 Oktoba, 2025.

DKT.SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI JIJINI MWANZA

October 07, 2025 Add Comment

Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Mwanza katika muendelezo wa Kampeni za Uchaguzi kwa CCM mkoanI Mwanza tarehe 07 Oktoba, 2025.

Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi waliofika kumpokea katika uwanja wa Ndege wa Mwanza tarehe 07 Oktoba, 2025.

Shamra shamra za mapokezi ya Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Mwanza tarehe 07 Oktoba, 2025.