DKT.BITEKO AWAASA WATANZANIA KUPIGA KURA OCTOBA 29

October 05, 2025


📌 *Rais Samia kuzulu Bukombe wiki ijayo*


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ametoa wito kwa Watanzania waliojiandikisha kupiga kura kujitokeza kwa wingi Oktoba 29 mwaka huu, ili kuwachagua viongozi wao katika  nafasi ya Urais, Ubunge na Udiwani.


Dkt. Biteko amesema hayo leo Oktoba 5, 2025 alipopewa nafasi ya kusalimia wakati ibada ya jumapili katika Kanisa la AICT Ushirombo, Bukombe mkoani Geita.

“ Natoa wito kwa wote wakiojiandikisha kupiga kura, Oktoba 29 wajitokeze kwa wingi kwa sababu kura yako ni haki ya kikatiba na ina uhusiano wa moja kwa moja na maendeleo yako,” amesema Dkt. Biteko.


Amebainisha kuwa katika zoezi la upigaji kura kutakuwa na vituo vingi vya kupiga kura ili kurahisisha ushiriki wa wananchi.


Fauka ya hayo, Dkt. Biteko amewaeleza waumini wa Kanisa hilo la AICT kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wiki ijayo atakuwa wilayani Bukombe hivyo amewaomba kujitokeza na kushiriki katika mapokezi yake.

“Naomba mpokee salamu nyingi za Mhe. Rais Samia ambaye Oktoba 12 atakuwepo katika Wilaya yetu ya Bukombe, nawaomba mjitokeze kwa wingi kwa ajili ya kumkaribisha kwa kuwa Mhe. Rais anatupenda sana.” Amemaliza Dkt. Biteko. 


Mwisho

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »