Na Oscar Assenga, TANGA.
HATIMAYE Reli iliyokuwa ikitoka Bandari ya Tanga kupitisha shehena za Mizigo kuelekea mikoa mbalimbali ikiwemo ya Kanda ya Kaskazini ambayo ilisimama kufanya kazi kwa kipindi cha miaka 20 imezinduliwa rasmi kuanza kuendelea na huduma zake baada ya kufanyiwa maboresho makubwa.
Halfa ya uzinduzi wa Reli hiyo ulifanywa Octoba 7 mwaka huu na Meneja wa Bandari ya Tanga Selehe Mbega ikiwa ni muendelezo wa wiki ya huduma kwa wateja ambapo wadau mbalimbali ikiwemo kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC) pamoja na watumishi wa Bandari hiyo walishuhudia uzinduzi huo.
Akizungumza mara baada ya kuizindua, Meneja wa Bandari ya Tanga Salehe Mbega aliishukuru Serikali kwa kuwekeza kwenye maboresho ya reli hiyo ambayo kwa sasa imeanza kutumika kupitisha shehena kutoka Bandari kwenye mikoa mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi.
Alisema kufufuliwa kwa reli hiyo kumeandika historia ya kuanza kufanya kazi kutokana na kwa kawaida usafirishaji bidhaa kutoka Bandarini ni rahisi kufanyika kutumia treli na barabara.
Aidha alisema lakini wanafahamu kwenye barabara uwezo unakuwa mdogo sana hivyo utumiaji wa treni unasaidia katika kuhudumia shehena nyingi kwa wakati mmoja na hivyo kurahisisha shughuli. Na kwa sasa shehena zitakuwa zinasafirisha kwenye bandari hiyo .
Hata hivyo alisema kwamba pia Bandari hiyo imeweka rekodi mpya kwa kukusanya kiasi cha Bilioni 31 kwa kipindi cha miezi mitatu katika kipindi cha robo ya kwanza kuanzia Julai hadi Septemba kiwango ambacho hakikuwahi kukusanywa tokea Bandari hiyo ifanye operesheni zake.
Aliongeza kwamba njia hiyo ya kusafirisha shehena kupitia reli kitakuwa na tija kutokana na kwamba itabeba mizigo mkubwa kutoka Tanga kuelekea magharibi ya nchi kama vile Kigoma, Mwanza na n chi jirani za Rwanda na Burundi.
Alitoa wito kwa wafanyabiashara ambao wanasafirisha bidhaa zao kwenda nchi za Rwanda,Burundi na mikoa ya jirani ya Kigoma na mwanza kutumia Bandari ya Tanga kwa sababu ya urahisi wa usafirishaji kwa njia ya reli ambapo mzigo mkubwa unaweza kusafirishwa kwa pamoja.
“Lakini pia kwa gharama nafuuu hivyo wateja wetu usafiri wa treni sasa unapatikana tunawashauri muendelee kutumia Bandari ya Tanga kutokana na maboresho makubwa yaliyofanyika “Alisema
Meneja huyo alisema katika Bandari hiyo imefunguka idadi ya meli imeongeze, shehena imeongezeka miaka mitatu au mine iliyopita hali haikuwa hivyo lakini sasa mizigo imekuwa mingi Bandari na ukipita barabarani malori ni mengi .
Awali akizungumza katika halfa hiyo, Meneja wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Mkoa wa Tanga Laurance Themanini aliipongeza Serikali inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu katika ziara yake aliyoifanya mkoani Tanga mwaka huu huku akieleza kwamba Bilioni 1 wametumia kurudisha miundombinu ya reli katika Bandari.
Alisema katika ziara hiyo alitoa maagizo kwamba miundombinu ya reli iunganishwe na Bandari ili kutoa huduma kwa wananchi wa Tanzania ambapo alisema agizo hilo wamelitekeleza na sasa wameshaanza kutoa huduma kwa wadau wanaotumia reli kusafirisha mizigo kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa,Nyanda za Juu na Mikoa ya Kanda ya Kaskazini.
Alisema na mpaka sasa wamekwisha kusafrisha mizigo tani 1500 kutoka Bandari ya Tanga kupeleka mikoa ya Kanda ya Ziwa na wanatarajiwa kupata wateja wengi na watasafirisha shehena kubwa sana wanaweza kusafirisha tani 30,000 kwa mwaka mmoja huku akiwakaribisha watanzania kutumia Badnari hiyo kusafirisha.
Mwisho.
EmoticonEmoticon