KUELEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIA MACHI 8 MBUNGE UMMY MBUNGE WA KWANZA MWANAMKE JIMBO LA TANGA
siasaNA: MWANDISHI WETU, TANGA
Tarehe 08 Machi ya kila mwaka ni Siku ya Wanawake Duniani. Siku hii imebeba tafakuri ya kina juu ya mchango wa mwanamke katika kuchochea maendeleo ya nyanja zote; kijamii, kiuchumi na kisiasa. Pia, ni siku ya kujadili changamoto zinazowakabili wasichana na wanawake ili kuzitatua kama msingi wa kuharakisha maendeleo. Wanawake ni wadau muhimu wa maendeleo na bila ushiriki wao ipasavyo, juhudi hizo hazitazaa matunda yanayotarajiwa, ndiyo maana jamii inapaswa kuwashirikisha wasichana na wanawake kikamilifu.
Sambamba na hilo, wanawake wamekuwa wakihamasishwa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kama Udiwani, Ubunge na hata Urais ili wapaze sauti zao wenyewe moja kwa moja badala ya kutegemea kusemewa na wanaume au kutegemea uwepo wa nafasi za viti maalum kwenye Udiwani na Ubunge. Ummy Mwalimu, Mbunge wa Tanga Mjini, ni mfano wa wabunge wanawake katika Bunge la Tanzania walioamua kugombea na kushinda ubunge mwaka 2020.
Ummy Mwalimu ambaye kitaaluma ni Mwanasheria, alianza kuwa Mbunge wa viti maalum mkoa wa Tanga kwa vipindi viwili yaani mwaka 2010-2015 na baadaye 2015-2020. Mwaka 2020 aligombea rasmi Ubunge kuwakilisha wananchi wa Jimbo la Tanga Mjini ambapo aliibuka mshindi kwa kishindo kikubwa. Kwa hakika, Ummy Mwalimu ni kielelezo cha wanawake wenye uthubutu na kujiamini katika uongozi.
Kimsingi, Ummy Mwalimu amefanikiwa kuwa Mbunge wa mfano Bungeni kutoka na uchapakazi na uhodari wake wa kujenga hoja akiwasilisha vyema changamoto za wananchi wa Tanga Mjini ili viweze kufanyiwa kazi. Hata Wizara mbalimbali alizohudumu kama Waziri, amekuwa kielelezo kizuri cha uchapakazi uliotukuka.
Kwa mfano, Ummy Mwalimu amewahi kuwa Waziri wa Afya kwa vipindi viwili (2015-2020 na 2022-2024). Vilevile, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) mwaka 2021. Pia, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira na Naibu Waziri Katiba na Sheria (2010-2015). Nafasi hizo zote amezitumikia kwa ufanisi na kuacha matokeo mazuri kote alipohudumu.
![]() |
Sanjari na hilo, ni katika uongozi wake ambapo Jimbo la Tanga Mjini limepiga hatua kubwa za kimaendeleo hasa katika miradi mikubwa ya kimaendeleo na ya kimkakati. Mathalani, uboreshaji wa huduma za afya, elimu, maji, umeme, barabara, bandari, masoko, kilimo cha mwani, utoaji wa mikopo kwa wanawake, vijana na wenye mahitaji maalum na huduma nyingine nyingi. Ummy Mwalimu amethibitisha uwezo mkubwa wa kiuongozi walionao wanawake katika kuwatumikia wananchi. Huyu ndiye Ummy Mwalimu, kwa jina maarufu "Odo Ummy."
Ikumbukwe kuwa kilele cha Siku ya Wanawake Duniani ni Tarehe 08 Machi ya kila mwaka ambapo kwa mwaka huu 2025, maadhimisho hayo yatafanyika mkoani Arusha, yakichagizwa na kaulimbiu isemayo: Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji; huku Mgeni Rasmi akitarajiwa kuwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.
RC BALOZI BATILDA AWAOMBA VIONGOZI WA DINI WAHIMIZE WAUMINI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA
siasaNa Oscar Assenga,Tanga
KATIBU WA SUKI RABIA -KILICHOFANYWA NA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU HAKIJAVUNJA KATIBA YA CHAMA
siasaNA WILLIUM PAUL, ROMBO.
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi na Katibu wa Nec Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Rabia Hamid amesema kuwa kilichofanywa na Wajumbe wa Mkutano mkuu kumpitisha Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa Chama hicho katika uchaguzi mwaka huu ni kwa mujibu wa katiba ya Chama.
Rabia ambaye ni mlezi wa Chama hicho mkoa wa Kilimanjaro alitoa kauli hiyo jana wakati wa maadhimisho ya miaka 48 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi ambapo kimkoa yamefanyika kata ya Katangara mrere wilayani Rombo.
Alisema kuwa, wapo baadhi ya wanasiasa ambao wamekuwa wkaipotosha kuwa kilichofanyika na Wajumbe hao ni kukiuka katiba ya chama na kuwataka wanaccm na wananchi kuwapuuza.
"Mkutano mkuu wa Chama cha Mapinduzi ndio chombo cha mwisho cha maamuzi na kilichofanywa na Wajumbe wake kimezingatia katiba ya Chama hivyo wapuuzeni hao wanaoibuka na kutoa taarifa za uongo" Alisema Rabia.
Mjumbe huyo wa Nec alisema kuwa, kwa sasa Chama hicho kinaenda kujipanga kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025 ili kuhakikisha wagombea wake wanashinda kwa kishindo na Tanzania inaenda kuwa ya kijani.
Alisema kuwa, kwa sasa wameshawahesabu wapiga kura wa ccm na uchaguzi wa mwaka huu Chama kitaenda kushinda kwa kishindo na kuwataka Wapinzani kukaa mkao wa kula.
Rabia alisema kuwa, hakuna chama chenye historia kama CCM na uimara wake ambapo wananchi wamekuwa wakikituma kupitia viongozi wake na wao wapo tayari kutumwa na kuwatumikia wananchi.
"Wananchi mnawajibu wa kumuongezea moyo wa kutafuta fedha nyingi zaidi za maendeleo kwa kumpa kura nyingi za kishindo pamoja na kuilinda na kuitunza miradi inayotekelezwa ili iweze kudumu muda mrefu.
Kwa upande wake, Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa kupitia mkoa wa Kilimanjaro, Seleman Mfinanga alisema kuwa, miaka 48 ya kuzaliwa kwa chama hicho yapo mafanikio makubwa ya kujivunia katika kipindi chote hicho.
"Miaka 48 ya CCM tumeshuhudia ujenzi wa miradi mikubwa ya maendeleo katika sekta mbalimbali za elimu, Afya, Barabara, maji na hili ni jambo la kujivunia katika miaka 48 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi" Alisema Mfinanga.
RAIS SAMIA AMEING'ARISHA CHAMWINO KIMAENDELEO -DKT BITEKO
siasa📌Serikali imewekeza zaidi ya bilioni 13 elimu ya Sekondari Chamwino
📌Uboreshaji wa miundombinu shilingi bilioni 17.9 zimetumika
📌Vijiji vyote 47 Chamwino vimewashwa umeme
📌Asema Sekta ya Nishati ipo salama
*Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati*
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa ya kuing'arisha Chamwino kwa kutatua changamoto mbalimbali za wananchi wa Jimbo hilo.
Hayo yamebainishwa leo Februari 02, 2025 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma mara baada ya uwasilishwaji wa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa kipindi cha miaka 5, (2020 2025) iliyowasilishwa na Mbunge wa jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi.
![]() |
"Nimemsikiliza Mhe. Ndejembi akieleza kazi kubwa ambayo Serikali imeifanya hapa Chamwino, ni dhahiri kwamba Serikali ya CCM chini ya Uongozi wa Dkt. Samia imefanya kazi kubwa ya kuing'arisha Chamwino na kutatua changamoto mbalimbali za wananchi wa Jimbo hili. Hongereni sana, " Amesema Mhe. Biteko
Aidha, amewataka kuendelea kuisimamia Serikali kuanzia ngazi ya chini ili kuendelea kuyagusa maisha ya wananchi kikamilifu na kutatua kero na changamoto walizonazo.
"Ni ukweli usiopingika kwamba Serikali ya CCM imefanya kazi kubwa sana na ya kutukuka ya kuiletea nchi yetu maendeleo. Ninyi hapa Chamwino ni mashahidi wakubwa wa maendeleo yaliyofanywa na Serikali chini ya Uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan," ameongeza Dkt. Biteko.
Vile vile, Serikali imewekeza zaidi ya bilioni 13 katika kugharimia elimu ya Sekondari tu katika Wilaya ya Chamwino.
"Tunashuhudia kuendelea kukamilika kwa ujenzi wa Shule hii ya Mkoa ya Sekondari ya ya Bweni ya Wasichana Manchali ambapo Watanzania wote watapata huduma za elimu," ameongeza Dkt. Biteko
![]() |
Katika hatua nyingine amesema kuwa, uboreshaji wa miundombinu kwa kujenga madaraja, vivuko na barabara za lami ndani ya Jimbo la Chamwino zaidi ya Shilingi bilioni 17.9 zimetumika.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Alhaj, Adam Kimbisa amewahimiza wakazi wa Chamwino kuendeleza umoja na mshikamano miongoni mwao ili kulinda madanikio yaliyofikiwa.
Pia, amewata kutumiia mvua za msimu kulima kwa wingi na watakapopata mavuno wahifadhi sehemu ya mavuno yao ili kuwa na akiba ya chakula kwa siku zijazo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Deogratius Ndejembi amesema kuwa jitihada za Rais Samia kutoa fedha za miradi zimechangia kuharakisha maendeleo ya jimbo ikiwemo usambazaji wa nishati ya umeme kwa wananchi.
"Kata zote 14 zenye vijiji 47 zimewashwa umeme ambapo kazi hiyo imefanyika katika kipindi cha kuanzia mwaka 2021 hadi 2024," amesema Mhe. Ndejembi.