WATAALAM SADC WAKUTANA ZIMBABWE KUJADILI SEKTA YA NISHATI NA MAJI

June 30, 2025


📌 *Miundombinu ya usafirishaji umeme kikanda kujadiliwa*


📌 *Nishati Safi ya kupikia kupewa kipaumbele*


📌 *Mkakati mahsusi wa kuongeza watumiaji wa umeme Afrika (M300) kuwa moja ya Ajenda*


📌 *Maendeleo ya Sekta ndogo ya Mafuta na Gesi pamoja na umeme vijijini kujadiliwa*



Wataalam wa Wizara ya Nishati pamoja na taasisi zake  leo wameshiriki katika Mkutano wa ngazi ya  Makatibu Wakuu na Watalaam wanaoshughulikia masuala ya Nishati na Maji unaofanyika katika Jiji la Harare nchini Zimbabwe. 

Mkutano huo wa awali ni sehemu ya maandalizi kuelekea katika Mkutano wa pamoja wa Kamati ya Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Nishati na Maji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). 


Mkutano huo pamoja na kujadili masuala ya Nishati na Maji, umekuwa ni fursa pia kwa Tanzania  kuendeleza diplomasia ya kiuchumi pamoja na kuwasilisha mafanikio ya nchi katika kuboresha huduma za nishati vijijini kupitia miradi inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijjni (REA). 

Aidha, Mkutano huo umeangazia maendeleo ya Sekta ndogo ya Mafuta na Gesi, pamoja na ujenzi wa miundombinu ya kikanda ya Mafuta na gesi inayohusu nchi wanachama wa SADC. 

Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na taasisi zake waliohudhuria mkutano huo ni Kamishna Msaidizi wa Maendeleo ya Umeme, Mha. Styden Rwebangila, Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mha. Hassan Saidy, Mkurugenzi wa  Mipango na Uwekezaji (TPDC), Derick Moshi, Mkurugenzi wa Mifumo ya Udhibiti Umeme (TANESCO) , Mha. Deogratius Mariwa, Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi (EWURA), Msafiri Mtepa na  Wataalam kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »