Timu ya Mamlaka ya hifadhi ya eneo la (Ngorongoro) imeagwa leo tarehe 4 Novemba, 2026 kuelekea mkoani Morogoro kushiriki mashindano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) ambapo imesafiri ikiwa na ari ya kurudi na ushindi mnono kupitia michezo ya mpira wa Miguu, Netbali, Vollebal, Kamba na Michezo ya Jadi na Kuahidi kurudi na vikombe.
Akizungumza kwa niaba ya kamishna wa Uhifadhi wakati akiwaaga wachezaji hao, Naibu Kamishna huduma za Shirika, Bw. Aidan Makala , amewaasa washiriki kuzingatia nidhamu ya hali ya juu katika kipindi chote cha mashindano, akisisitiza kuwa nidhamu, umoja na ushirikiano ni msingi muhimu wa mafanikio katika michezo.
“Mnapoenda kushiriki michezo mnaitangaza Ngorongoro kupitia utalii wa michezo, ni mategeo yangu kuwa mtakuwa mabalozi wa Ngorongoro, kuzingatia nidhamu, maadili na sheria za nchi na kuhakikisha kuwa timu yetu inarudi na vikombe vya kutosha”amesisitiza Makala



EmoticonEmoticon