RAIS SAMIA, RAIS JOÃO, WAZINDUA KILOMITA 59.1 ZA BARABARA ZA LAMI MJI WA SERIKALI MTUMBA

October 30, 2026

 


Na: OWM–TAMISEMI, Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, na Rais wa Jamhuri ya Angola, Mhe. João Lourenço, leo Oktoba 30, 2026, wamezindua barabara za Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma, zinazowawezesha wananchi kufika katika Wizara na Taasisi za Serikali kupata huduma zinazotolewa na taasisi hizo za umma.

Akitoa taarifa kuhusu barabara hizo zilizojengwa na TARURA, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI), Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, amesema barabara hizo zina urefu wa kilomita 59.1 ambapo kati ya hizo, kilomita 11.7 ni za njia mbili na kilomita 36 ni za njia moja.
 Aidha, ili kuzuia mafuriko katika Mji wa Serikali, tumejenga mabwawa matatu ya kuzuia mafuriko,” ameeleza Prof. Shemdoe.

Sanjari na hilo, Prof. Shemdoe amewashukuru Marais hao kwa kukubali kushiriki uzinduzi wa barabara hizo, huku akimshukuru kipekee Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wake wa kuzipa baadhi ya barabara majina ya viongozi wakuu wa kitaifa waliopita, akiwemo Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiwa na Rais wa Jamhuri ya Angola, Mhe. João Lourenço, leo Oktoba 30, 2026, pia amezindua rasmi majengo ya ofisi za Wizara na Taasisi za Serikali na baada ya uzinduzi huo amezungumza na wananchi wa Dodoma.












Share this

Related Posts

Previous
Next Post »