TANZANIA SASA INA ZIADA YA UMEME

November 10, 2026



Shinyanga.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungvano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema kukamilika kwa ujenzi wa Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere (JNHPP), lenye uwezo wa kuzalisha megawati 2,115, kumeimarisha upatikanaji wa umeme nchini na kuiwezesha Tanzania kuwa na ziada ya umeme.

Amesema hayo leo, Novemba 9, 2026, wakati wa ziara yake mkoani Shinyanga, inayoendelea kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

Ameeleza kuwa kukamilika kwa mradi huo ni matokeo ya maamuzi ya kimkakati yaliyofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuhakikisha miradi mikubwa ya kimkakati inakamilika.

Aidha, Waziri Mkuu amebainisha kuwa kutokana na maamuzi hayo, baadhi ya miradi ya maendeleo ilisimamishwa kwa muda, ikiwemo miradi ya barabara, maji na umeme, ili kuwezesha Serikali kuelekeza nguvu katika kukamilisha mradi huo mkubwa wa uzalishaji wa umeme.

Amesisitiza kuwa kwa sasa matokeo ya maamuzi hayo yanaonekana kupitia uzalishaji wa umeme unaochangia kuimarisha uhakika wa nishati nchini.


Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »