PSSSF YAKABIDHI MIRADI YA MAJI SHULE MBILI DODOMA

November 05, 2026


Meneja wa Mfuko wa PSSSF Kanda ya Kati, Bw. Lulyaya Sayi (Aliyesimama) akizungumza katika hafla ya kukabidhi mradi wa kisima Cha maji katika Shule ya Sekondari Kimaghai A, Wilayani Mpwapwa jijini Dodoma Novemba 4, 2026.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Bw. Ally Akida (Wapili kushoto), Meneja wa Mfuko wa PSSSF Kanda ya Kati, Bw. Lulyalya Sayi (Wanne kushoto), na Mkuu wa Shule ya Sekondari Kimaghai A, Bi. Eudia Medaa (Watano kushoto) na baadhi ya viongozi wa wilaya na walimu wa shule hiyo, wakiungana kuzindua, mradi wa maji uliofadhiliwa na Mfuko wa PSSSF katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika shuleni hapo Novemba 4, 2026

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Bw, Ally Akida (Aliyesimama) akizungumza katika hafla ya kukabidhi mradi wa kisima Cha maji uliofadhiliwa na Mfuko wa PSSSF katika Shule ya Sekondari Kimaghai A, jijini Dodoma. Hafla hiyo imefanyika Novemba 4, 2026.

Meneja wa PSSSF Kanda ya Kati, Bw, Lulyaya Sayi, Kaimu Afisa Elimu wa Halmashauri ya mji Dodoma Bw, Yasin Mponda, Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru wakishuhudia uwepo wa maji kwa uhakika baada ya kukamilika kwa mradi huo katika Shule ya Msingi Uhuru.
Picha ya pamoja ikionyesha Meneja wa PSSSF Kanda ya Kati, Bw. Lulyaya Sayi, Kaimu Afisa Elimu wa Halmashauri ya Mji wa Dodoma, Bw. Yassin Mponda, Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru, Bi. Agatha Mosha, pamoja na watumishi, wazazi, na wanafunzi waliohudhuria katika uzinduzi wa mradi wa maji katika Shule ya Msingi Uhuru.
Kaimu Afsa Elimu wa Halmashauri ya Mji wa Dodoma, Bw, Yasin Mponda akizungumza katika hafla ya kukabidhi mradi mradi wa kisima Cha maji katika Shule ya Msingi Uhuru, Dodoma.

Meneja wa PSSSF Kanda ya Kati, Bw, Lulyaya Sayi akizungumza katika hafla ya kukabidhi mradi wa kisima Cha maji katika Shule ya Msingi Uhuru.


*Miradi Kunifaisha zaidi ya Watu 1000

*Wanafunzi Waanzisha Bustani Kuboresha Lishe

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umekabidhi miradi miwili ya visima vya maji vyenye thamani ya Shilingi milioni 55 katika Shule ya Sekondari Kimaghai, Mpwapwa, na Shule ya Msingi Uhuru, jijini Dodoma, inayotarajiwa kunufaisha zaidi ya watu 1,000.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya mradi wa Kimaghai A, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Bw. Ally Akida, aliishukuru PSSSF kwa kutatua changamoto ya muda mrefu ya maji, akieleza kuwa mradi huo utanufaisha zaidi ya watu 600.

Naye Kaimu Afisa Elimu wa Jiji la Dodoma, Bw. Yasin Mponda, aliipongeza PSSSF kwa kukubali  ombi la Shule ya Msingi Uhuru, akieleza kuwa Mfuko umeifanya shule hiyo kujiona inathaminiwa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru, Bi. Agatha Mosha, aliishukuru PSSSF kwa mradi huo ambao umewezesha kuanzishwa kwa kilimo cha mbogamboga kwa ajili ya kuboresha lishe ya wanafunzi na unatarajiwa kunufaisha zaidi ya watu 500.

Makabidhiano ya miradi hiyo yalifanyika tarehe 3 na 4 Novemba 2026, yakiongozwa na Meneja wa PSSSF Kanda ya Kati, Bw. Lulyaya Sayi, aliyewataka wanafunzi, walimu na wananchi kutunza visima na miundombinu yake ili iendelee kutoa huduma kwa muda mrefu.


Share this

Related Posts

Previous
Next Post »