
Dodoma
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, amelipongeza Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mchango wake katika kusimamia utekelezaji wa Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) hadi kukamilika kwake kwa asilimia 100.
Mhe. Salome ametoa pongezi hizo wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Mwera, Mhe. Suleiman Mohamed Rashid, aliyetaka kujua lini Serikali itakamilisha Mradi wa Bwawa la Julius Nyerere.Akijibu swali hilo, Mhe. Salome amesema mradi huo ulikamilika kwa asilimia 100 Februari 23, 2025, na kuzinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Agosti 22, 2026.
Ameeleza kuwa kwa sasa mitambo yote ya mradi huo inafua umeme wenye jumla ya Megawati 2,115, ambao huingizwa kwenye Gridi ya Taifa kulingana na mahitaji ya umeme nchini.
EmoticonEmoticon