MHE.SALOME ATOA SIKU TANO KWA ETDCO KUKAMILISHA UJENZI WA KITUO CHA KUBORESHA HALI YA UMEME (AVR) NANYUMBU

November 12, 2026

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, ameiagiza kampuni tanzu ya TANESCO ya ETDCO kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Kuboresha Hali ya Umeme (AVR) kilichopo Mangaka, Wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara, ambacho kitaongeza nguvu ya  kuendesha mradi wa maji  na hivyo kuwawezesha wananchi kupata maji kwa ufanisi.

Kituo hicho cha AVR kinajengwa kwa lengo la kuimarisha kiwango cha volteji ya umeme unaosambazwa katika mradi wa maji wa Mangaka, hatua itakayosaidia mitambo ya kusukuma maji kufanya kazi kwa ufanisi na kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi.

Mhe. Salome ametoa agizo hilo leo, Novemba 12, 2026, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho unaotekelezwa na Kampuni ya ETDCO.

Amesisitiza kuwa kazi zote zilizosalia zinapaswa kukamilishwa ndani ya muda alioutoa ili kituo hicho kianze kufanya kazi.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »