
Na Mwandishi Wetu, Korogwe
WANAFUNZI wa Kike katika Shule za Sekondari nchini wametakiwa kusoma kwa bidii masomo ya sayansi ili kuwawezesha kupata ufadhili wa Samia Suluhu ambao utakuwa chachu kwao kuweza kufikia ndoto zao za kielimu.
Hayo yalisemwa leo na Mkurugenzi Kampuni ya Shemnyama African Association Business Consultancy and Insurance Agency Rajab Shemnyama ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa maafali ya kidato cha nne katika shule ya Sekondari Old Korogwe, Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga.
Ambapo alisema kwamba masomo ya sayansi yatawawezesha kukabiliana na ushindani wa soko la ajira kutokana na utandawazi uliopo

Alisema wanafunzi wanapaswa kutumia fursa za elimu kwa kujituma katika masomo ili shule hiyo iweze kuzalisha wataalamu wengi katika fani mbalimbali.
Pia, alisisitiza umuhimu wa matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii, akiwataka wanafunzi kuitumia kujifunza na kuongeza maarifa badala ya kujihusisha na mambo yanayoweza kuathiri maadili na maendeleo yao.
Aliwaasa kujiepusha na vitendo vya ukatili wa kijinsia na tabia hatarishi zinazoweza kuhatarisha afya na mustakabali wao, huku akisisitiza umuhimu wa kujitambua na kulinda heshima zao.
Aidha, alisema elimu inapaswa kwenda sambamba na ujuzi wa ziada utakaowawezesha vijana kujiajiri na kujipatia kipato, hasa kutokana na changamoto ya ajira inayoweza kuwakabili baada ya kuhitimu.
Alisisitiza kuwa wanafunzi wanapaswa kushiriki katika matamasha na shughuli za ujasiriamali ili kujenga uwezo wa kujitegemea kiuchumi.
Akizungumzia suala la chakula shuleni, Shemnyama aliwataka wazazi kushirikiana na walimu kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula cha mchana, akieleza kuwa njaa huathiri umakini na uwezo wa kufuatilia masomo darasani.

Pia, aliomba uongozi wa shule kuimarisha miradi ya kilimo ili kuongeza uzalishaji wa chakula na kuwajengea wanafunzi ujuzi wa kilimo, akibainisha kuwa sekta hiyo inaweza kuwa chanzo cha fursa mbalimbali za kiuchumi kwa vijana.
"Lakini pia kupitia Kampuni Yetu hii tutatoa madaftari kwa ajili ya watoto wasiokuwa na wazazi (Mayatima) kwa lengo la kuwapunguzia makali "Alisema
Alisema amezipokea changamoto zilizowasilishwa na uongozi wa shule hiyo na kuahidi kushirikiana na wadau wengine kutafuta namna ya kuzitatua.
Katika maafali hayo ameahidi kuchangia mifuko 20 ya saruji kwa ajili ya ukarabati wa maktaba ya Shule ya Sekondari Old Korogwe, Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia.

Mchango huo umetangazwa na Rajabu Shemnyama, ambaye ni mhitimu wa shule hiyo, wakati wa mahafali ya Kidato cha Nne, akisema hatua hiyo inalenga kuunga mkono juhudi za shule kuinua kiwango cha ufaulu na kuondoa daraja sifuri katika matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka 2026
Alisema amezipokea changamoto zilizowasilishwa na uongozi wa shule hiyo na kuahidi kushirikiana na wadau wengine kutafuta namna ya kuzitatua.
Katika maafali hayo ameahidi kuchangia mifuko 20 ya saruji kwa ajili ya ukarabati wa maktaba ya Shule ya Sekondari Old Korogwe, Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia.

Mchango huo umetangazwa na Rajabu Shemnyama, ambaye ni mhitimu wa shule hiyo, wakati wa mahafali ya Kidato cha Nne, akisema hatua hiyo inalenga kuunga mkono juhudi za shule kuinua kiwango cha ufaulu na kuondoa daraja sifuri katika matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka 2026
Shemnyama alisema ameamua kuchangia maendeleo ya shule hiyo kutokana na kutambua umuhimu wa elimu, akibainisha kuwa yeye ni zao la shule hiyo na anajivunia kuona mabadiliko yaliyofikiwa tangu alipokuwa mwanafunzi.
Alisema maendeleo ya elimu yanahitaji ushirikiano wa wadau mbalimbali, hivyo kuwataka wahitimu na watu wengine waliowahi kusoma katika shule hiyo kujitokeza kuchangia kuboresha mazingira ya kujifunzia.
Aliongeza kuwa kampuni yake itaendelea kushirikiana na shule hiyo katika shughuli za maendeleo, ikiwamo kuchangia madaftari kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Old Korogwe, Bilali Shemkai, alisema shule hiyo imeweka mikakati ya kuhakikisha hakuna mwanafunzi atakayepata daraja sifuri katika matokeo ya Kidato cha Nne mwaka 2026.
Alisema juhudi hizo zimeanza kuonyesha matokeo kutokana na kupungua kwa idadi ya wanafunzi waliopata daraja hilo kutoka 38 mwaka 2023 hadi 20 mwaka 2024 na 10 mwaka 2025.

Alisema mbali na kuondoa daraja sifuri, shule hiyo inalenga kuongeza idadi ya wanafunzi watakaopata madaraja ya kwanza, pili na tatu.
Shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2004 ina jumla ya wanafunzi 520, wakiwamo wasichana 284 na wavulana 236, pamoja na watumishi 32, wakiwamo walimu 31 na mtaalamu mmoja wa maabara.
Ina vyumba 14 vya madarasa na maabara tatu, ambapo maabara za Kemia na Baiolojia zimekamilika, huku maabara ya Fizikia ikiwa bado haijakamilika.
Pamoja na kuwa na huduma za maji, umeme na barabara, shule hiyo pia ina mradi wa kilimo unaohusisha uzalishaji wa mahindi na majaribio ya kilimo cha mpunga kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa chakula.

Hata hivyo, shule hiyo bado inakabiliwa na changamoto ya kuhakikisha wanafunzi wote wanapata chakula cha mchana, hali inayoufanya uongozi kuendelea kuwahamasisha wazazi kushiriki katika uchangiaji wa chakula.
Kupitia utaratibu uliowekwa, kila mzazi anahamasishwa kuchangia kilo nane za mahindi, kilo mbili za maharage na Sh4,000 kwa kila muhula kwa ajili ya chakula cha wanafunzi. Hata hivyo, utekelezaji wake umekuwa na changamoto kutokana na mwitikio mdogo wa baadhi ya wazazi.
Changamoto nyingine ni uchakavu wa baadhi ya vyumba vya madarasa na mazingira ya nje ya shule, ambayo wakati mwingine yanaweza kuathiri utulivu na maandalizi ya wanafunzi kitaaluma.
Kutokana na hali hiyo, shule imekuwa ikishirikiana na viongozi wa serikali za mitaa na kata kukabiliana na changamoto zinazoweza kuathiri usalama na maendeleo ya wanafunzi.
Uongozi wa shule hiyo unaamini kuwa ushirikiano kati ya wazazi, walimu, wanafunzi, wahitimu na wadau wengine wa elimu utasaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia, pamoja na kufanikisha malengo ya kuinua ufaulu.






EmoticonEmoticon