DKT.HOMERA ASHIRIKI KIKAO CHA MARAIS WA TANZANIA NA UGANDA ENTEBBE

November 18, 2026


Uganda

Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera,  ameshiriki kikao cha mazungumzo kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, na Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, kilichofanyika leo katika Ikulu ya Entebbe, nchini Uganda.

Katika kikao hicho, imeelezwa kuwa Tanzania na Uganda zimepiga hatua katika utekelezaji wa makubaliano na maamuzi ya awali yaliyolenga kuimarisha ushirikiano wa nchi hizo katika sekta mbalimbali, zikiwemo biashara, uwekezaji, nishati, usafiri na miundombinu.

Katika sekta ya nishati, Tanzania na Uganda zinaendelea kushirikiana katika utekelezaji wa Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), lenye urefu wa kilomita 1,443 kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani, mkoani Tanga, Tanzania. Ushirikiano huo pia unahusisha ujenzi wa kituo cha kikanda cha nishati mkoani Tanga.

Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Ma-Katibu Wakuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio (Mafuta na Gesi) na Dkt. Felchesmi  Mramba (Umeme na Nishati Jadidifu).

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »