SERIKALI INATHAMINI WAJASIRIAMALI WADOGO NA WA KATI KUINUA BIASHARA ZAO

October 02, 2026
-Azindua Kitabu cha mwongozo wa bei za keki kwa waokaji nchini;

-Asema sekta ya uoakaji ina ajiri wajasiriamali wengi kwenye soko la ajira

Dar es salaam

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Judith Kapinga(Mb), Leo amezindua Kitabu cha mwongozo wa upangaji bei za keki kilichoandaliwa na mmoja wa wajasiriamali hapa nchini bi Tahya au Leymax,ambapo amempongeza Leymax kwa kutoa mchango kwa wajasiriamali wengi hapa nchini.

Mhe Kapinga amesema vijana wengi hususani wanawake na wanaume wamepitia mkono ya Mjasiriamali huyo kwa kupata elimu na ujuzi wa mafunzo ya Mjasiriamali huyo kupitiabujuzi wake wa utengenezaji keki.

‘’ Serikali inathamini mchango mkubwa unaotolewa na wajasiriamali wadogo na wa Kati hapa nchini ma tunaahidi kuweka mazingira mazuri ya biashara kwa waokaji’’ Alisema Mhe Kapinga.

Kwa upande wake Bi Tahya alimshukuru Mhe Kapinga kwa kuitikia wito wa kushiriki Uzinduzi wa Kitabu hicho kwani kitakuwa chachu ya kuleta mabadiliko kwa sekta ya waokaji keki hapa nchini na kuahidi kufungua fursa zaidi kwa wajasiriamali.

Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »