
Mkurugenzi wa Idara ya Elimu ya Sekondari Zanzibar, Asya Iddi Issa, akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa Jukwaa la Elimu ya Teknolojia (EdTech) la mwaka 2026, lililoandaliwa chini ya Mpango wa Mafunzo na Elimu Kazini (INSET), unaolenga kuimarisha uwezo wa walimu katika kutumia teknolojia na mbinu za kidijitali kuboresha ufundishaji na ujifunzaji. Hafla hiyo imefanyika katika Kituo cha Kitaifa cha Rasilimali Walimu (NTRC), Kiembe Samaki, Zanzibar, Alhamisi, Septemba 17, 2026. Jukwaa hilo, lenye kaulimbiu “Kuonesha Ujifunzaji wa Kidijitali, Ubunifu na Mustakabali wa Elimu Zanzibar”, limeandaliwa na Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete (JMKF) kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar (MoEVT), Lyra Africa pamoja na shule 10 za sekondari zinazoshiriki katika mradi huo. Kushoto ni Bi Vivian Koka wa JMKF na kulia ni Bi Trust Mwalyango wa JMKF pia.
.jpeg)
Mkurugenzi wa Idara ya Elimu ya Sekondari Zanzibar, Asya Iddi Issa, akiwa katika picha na washiriki na waandaji wa Jukwaa la Elimu ya Teknolojia (EdTech) la mwaka 2026, lililoandaliwa chini ya Mpango wa Mafunzo na Elimu Kazini (INSET), unaolenga kuimarisha uwezo wa walimu katika kutumia teknolojia na mbinu za kidijitali kuboresha ufundishaji na ujifunzaji. Hafla hiyo imefanyika katika Kituo cha Kitaifa cha Rasilimali za Walimu (NTRC), Kiembe Samaki, Zanzibar, Alhamisi, Septemba 17, 2026. Jukwaa hilo, lenye kaulimbiu “Kuonesha Ujifunzaji wa Kidijitali, Ubunifu na Mustakabali wa Elimu Zanzibar”, limeandaliwa na Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete (JMKF) kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar (MoEVT), Lyra Africa pamoja na shule 10 za sekondari zinazoshiriki katika mradi huo. Kulia kwake ni Bi Vivian Koka wa JMKF na Mkuu wa Kituo cha Kitaifa cha Rasilimali Walimu Bw. Mohamed Khamis Suleiman na kushoto kwake ni Bi Trust Mwalyango wa JMKF.
ZANZIBAR — Septemba 17, 2026: WalimuvisiwaniZanzibar wamehimizwakutumiateknolojia kwa vitendokatikaufundishajiwakila siku,badalayakujadilituumuhimuwaujifunzajiwakidijitali.
Wito huo umetolewa na Mkurugenziwa Idara ya Elimu ya Sekondari Zanzibar, Asya Iddi Issa, wakati akifungua rasmi mafunzo ya Jukwaa la EdTech la kwanza kufanyika visiwani, lililoandaliwa chini ya Mpango wa Mafunzo na Elimu Kazini (INSET)unaolenga kuimarisha uwezo wa walimu katika kuboresha ufundishaji.
Jukwaa hilo liliandaliwa na Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete (JMKF),kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar (MoEVT), Lyra Africa na shule 10 za sekondari zinazoshiriki katika mradi huo.
Jukwaa hilo lilifanyika katika Kituo cha Kitaifa cha Rasilimali za Walimu (NTRC), Kiembe Samaki, Zanzibar, likiwa nakauli mbiu: “Kuonesha Ujifunzaji wa Kidijitali, Ubunifu na Mustakabali wa Elimu Zanzibar.”
Bi. Issa alisema walimu wengi tayari wanamiliki vifaa vya kisasa vya kidijitali, lakini vifaa hivyo havitumiki kikamilifu katika ufundishaji, utafiti na maendeleo yao ya kitaaluma.
“Walimu wanapaswa kufanya kila linalowezekana kutekeleza kwa vitendo yale wanayojifunza. Pia wanapaswa kufanya juhudi za makusudi kuelewa na kukubali matumizi ya teknolojia,badala ya kuwategemea walimu wa TEHAMA pekee,” alisema.
Alisisitiza kuwa ujumuishaji wa teknolojia ni jukumu la walimu wote, akiwataka kutumia simu na kompyuta kuandaa masomo, kutafuta maarifa, kuboresha ufundishaji na kuwasaidia wanafunzi kufikiri kwa upana zaidi.
“Vifaa vya kidijitali vilivyo mikononi mwetu havipaswi kubaki kwaajili ya kupiga simu, kutuma ujumbe na burudani pekee. Vinapaswa kuwa zana za kuandaa masomo, kutafuta maarifa, kuboresha ufundishaji na kuwasaidia wanafunzi kufikiri kwa upanazaidi,” alisema.
Pia aliwahimiza walimu na wanafunzi kutumia akili bandia (AI) kama nyenzo yakufanya utafiti, kupata vifaa vya kujifunzia, kuzalisha mawazo na kupanua maarifa. Hata hivyo, alionya kuwa teknolojia hiyo haipaswi kutumiwa kuendeleza udanganyifu wa kitaaluma, ikiwemo kufanya udanganyifu katika mitihani, kunakilikazi za watu wengine au kuandaa tasnifu na kazi za shule bila ushiriki wakweli wa mhusika.
“Akili bandia inapaswa kusaidia ujifunzaji, si kuchukua nafasi ya juhudi, uadilifu au fikra tunduizi,” alisema.
Jukwaa hilo liliwakutanisha maafisa wa wizara, maafisa waelimu, wakuu washule, walimu wa TEHAMA, viongozi wa Jumuiya za Kujifunza kwa Pamoja, wanafunzi na washirika wa utekelezaji kutoka shule 10 zinazoshiriki katika mradi huo.
Wakati wa jukwaa hilo, wanafunzi kutoka shule mbalimbali za sekondari walionesha ubunifu wao wa kidijitali, vipaji na mafanikio ya ujifunzaji, wakitoa mfano wa vitendo wa matumizi yanayoongezeka ya teknolojia katika elimu Zanzibar.
Wakati wa jukwaa hilo, wanafunzi kutoka shule mbalimbali za sekondari walionesha ubunifu wao wa kidijitali, vipaji na mafanikio ya ujifunzaji, wakitoa mfano wa vitendo wa matumizi yanayoongezeka ya teknolojia katika elimu Zanzibar.
EmoticonEmoticon