TRA YAWATAKA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUZINGATIA SHERIA ZA KODI

September 26, 2026
Kariakoo, 25 Septemba, 2026

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mkoa wa Kikodi Kariakoo, imewataka wafanyabiashara wa Kariakoo kutumia fursa ya Kariakoo Festival 2026 kupata elimu kuhusu masuala ya kodi, ikiwemo haki na wajibu wao kama walipakodi, huku ikisisitiza umuhimu wa uzingatiaji wa hiari wa sheria za kodi.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kariakoo Festival 2026 katika eneo la Sokoni-Kariakoo, Meneja wa Mkoa wa Kikodi Kariakoo, Bw. Edson Issanya, amesema TRA itaendelea kutoa elimu, kusikiliza changamoto na kuboresha huduma kwa walipakodi, huku akiwahimiza wafanyabiashara kutimiza wajibu wao wa kikodi kwa wakati, ikiwemo kulipa kodi ya awamu ya tatu kwa mwaka 2026 ambayo mwisho ni tarehe 30.

Aidha, banda la TRA litakuwepo katika maonesho kuanzia tarehe 25 hadi 30 Septemba 2026, likitoa fursa kwa wafanyabiashara na wananchi kupata elimu, ushauri na huduma mbalimbali za kikodi, pamoja na ufafanuzi kuhusu haki na wajibu wao kama walipakodi.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »