WAZIRI DEUS SANGU AIPONGEZA PSSSF KUFIKISHA THAMANI YA MFUMO TRILIONI 16.96 NA KUIMARISHA HUDUMA KWA WASTAAFU

September 25, 2026

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu (katikati), akizungumza alipotembela bdna la mfuko wa hifadhi ya jamii kwa watumishi wa umma (psssf) kwenye maonesho ya 9 ya teknolojia ya madini mkoani geita. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Geita Bw. Mohammed Gombati na kushoto ni Kaimu Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa Magharibi, Bw. Nathan Makuchilo

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu (kushoto) akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea banda la PSSSF kwenye Maonesho ya 9 ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita. Anayemshuhudia ni Kaimu Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa Magharibi, Bw. Nathan Makuchilo

Geita, Septemba 24, 2026 — Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, ameupongeza Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kuwa mfano wa kuigwa kutokana na mafanikio makubwa katika kuimarisha thamani ya mfuko na kuboresha huduma kwa wanachama na wastaafu.

Mhe. Sangu ameyasema hayo alipotembelea banda la PSSSF kwenye Maonesho ya 9 ya Teknolojia ya Madini Mjini Geita akibainisha kuwa  katika kipindi cha uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, thamani ya mfuko imepanda kutoka Shilingi Trilioni 7.4 Serikali ilipoingia madarakani hadi Shilingi Trilioni 16.96 hivi sasa. “Ongezeko hilo la zaidi ya mara mbili linaonesha uthabiti, uwazi na usimamizi thabiti wa rasilimali za wanachama,” amesema.


Kuhusu ulipaji wa mafao, amesema kupitia kaulimbiu ya “Tunalipa Jana,” wastaafu hupata mafao yao mara wanapostaafu na pensheni ya kila mwezi hulipwa kabla ya tarehe 25. Ameongeza kuwa PSSSF inashirikiana na waajiri kutoa elimu na kuwaandaa wastaafu, huku akisisitiza watumishi kujiandaa mapema kabla ya kustaafu ili kufanikisha malipo kwa wakati.


Kuhusu matumizi ya TEHAMA, Mhe. Sangu amesema PSSSF imewekeza kwenye mfumo wa PSSSF KIDIJITAL unaomwezesha mstaafu kuhakikiwa kidijitali akiwa popote alipo, hatua iliyoondoa adha ya kusafiri hadi ofisi za Mfuko kwa ajili ya uhakiki.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »