Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa akikabidhi tuzo ya Mdamini Mkuu wa Malkia wa Madini kwa Mkuu wa Kitengo cha Uendelezaji Biashara Changa na Ujumuishaji wa Kifedha, Ndugu, Fadhili Bushagama (kushoto) pamoja na Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana, wakati wa kilele chake kilichofanyika mkoani Geita, Septemba 25, 2025.
Mwenyekiti wa TAWOMA Taifa, Semeni Malale akizungumza katika wakati kilele cha usiku tuzo za Malkia wa Madini kilichofanyika mkoani Geita, Septemba 25, 2025.
Na Mwandishi Wetu.
Taasisi ya CRDB Bank Foundation imeshiriki katika kilele cha Malkia wa Madini 2026, kilichofanyika Septemba 25, 2026 mkoani Geita, katika hafla iliyoandaliwa na Tanzania Women Miners Association (TAWOMA) kwa lengo la kutambua, kuhamasisha na kuwezesha wanawake wanaoshiriki katika sekta ya madini.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Mgeni Rasmi, Mhe. Dkt. Steven Kiruswa, Naibu Waziri wa Madini, pamoja na viongozi na wadau mbalimbali kutoka katika sekta ya madini.
Akiwa mdhamini mkuu wa hafla hiyo, CRDB Bank Foundation imeendelea kusisitiza dhamira yake ya kuchangia uwezeshaji wa wanawake kiuchumi, hususan kupitia Programu ya Imbeju, inayolenga kuwawezesha wanawake na vijana kwa kuwapatia elimu ya fedha, kukuza ujasiriamali, kuwaunganisha na huduma za kifedha, pamoja na kujenga uwezo wa kuendeleza na kukuza shughuli zao za kiuchumi.
Ushiriki huu unaakisi dhamira ya CRDB Bank Foundation ya kushirikiana na wadau mbalimbali katika kujenga mazingira yanayowawezesha wanawake kushiriki kikamilifu katika uchumi, kutumia fursa zilizopo na kujenga shughuli endelevu zenye mchango katika maendeleo ya jamii.
CRDB Bank Foundation, Tunaamini katika uwezeshaji unaojenga uwezo, unaofungua fursa na kuleta mabadiliko endelevu kwa vijana na wanawake.











EmoticonEmoticon