“Nimeupokea kwa unyenyekevu na hamasa uteuzi wa kuwa Msemaji wa Sekta ya Fedha, Mipango na Hifadhi ya Jamii wa Kamati ya Wasemaji wa Kisekta ya ACT Wazalendo. Wajibu wangu ni kuzisimamia Wizara za Fedha chini ya Balozi Hamis Mussa Omar na Wizara ya Mipango na Uwekezaji chini ya Prof. Kitila Mkumbo.
Wizara hizi zimebeba taasisi nyeti kama vile Benki Kuu ya Tanzania na Sekta ya Benki kwa Ujumla wake, Hazina, TRA, Taasisi ya Manunuzi ya Umma (PPRA), TISEZA na Taasisi nyinginezo katika tasnia ya fedha na mipango.
Ninamshukuru Kiongozi wa Chama Ndugu Dorothy Semu kwa uteuzi huu. Nitatekeleza wajibu wangu kwa ufanisi, uadilifu na umadhubuti”- Ado Shaibu Ado.

EmoticonEmoticon