WAZIRI NDEJEMBI AFANYA KIKAO KAZI CHA PAMOJA NA TAASISI ZILIZO CHINI YA WIZARA YA NISHATI

April 07, 2026

 


Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi amekutana na kufanya kikao kazi cha pamoja na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati zinazoshughulikia mafuta leo Aprili 07, 2026 jijini Dodoma.


Lengo la kikao hicho ni kupitia na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu hali ya upatikanaji na bei za bidhaa za mafuta nchini itakayowasilishwa mbele ya kamati hiyo Aprili 08, 2026.

Kikao hicho kinatokana na agizo la Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Zungu alilolitoa Aprili 01, 2026 kwa Waziri wa Nishati akielekeza kukutana na Kamati ya Nishati na Madini ili kujadili hali na mwenendo wa kupanda kwa bei ya mafuta nchini.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi, Dkt. James Mataragio, Wataalamu kutoka wizarani pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya wizara zinazoshughulikia mafuta na gesi.



Share this

Related Posts

Previous
Next Post »