TUME YA MADINI YATOA UFAFANUZI KUHUSU AJALI KWENYE MGODI WA MSASA - GEITA

March 30, 2026
Ajali imetokea katika Mgodi wa Dhahabu wa Msasa uliopo Runzewe, Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, baada ya sehemu ya eneo la uchimbaji kuporomoka na kufunika madarura manne yenye namba K 46A, 47A, 48A na 49A.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Afisa Madini Mkazi – Mbogwe, madarura hayo yalikuwa yamefungwa tangu Machi 27, 2026 kwa ajili ya ukarabati, hata hivyo baadhi ya watu waliingia katika eneo hilo bila kufuata taratibu.

Taarifa imeeleza kuwa mvua kubwa zinazoendelea kunyesha zimechangia kulegea kwa udongo na kusababisha tukio hilo.

 Jitihada za uokoaji zilifanyika na hakuna kifo kilichoripotiwa.

Tume ya Madini imewataka wachimbaji na wananchi kuzingatia taratibu za usalama migodini ili kuepusha ajali kama hizi.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »