Na Oscar Assenga,TANGA
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira wametembelea maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa Maji wa Hatifungani ya Kijani (Green Bond) wenye thamani ya Sh.Bilioni 53.3 unaolenga kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma kwa wakazi wa Jiji la Tanga na wilaya za karibu
Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua miradi inayotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA) Machi 17,2026 Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Jackson Kiswaga alisema kwamba wameridhishwa na utekelezaji wa mradi huo
Mradi huo kwa sasa umefikia asilimia 65 ya utekelezaji wake na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Octoba mwaka huu ambao utakuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi.
“Kwa kweli tumetembelea mradi huu na tumeona namna unavyotekelezwa na kumeridhishwa nao kazi nzuri inaendelea “Alisema
Katika hatua nyengine Mwenyekiti wa Kamati hiyo alimpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu kwa kuruhusu ushiriki wa sekta binafsi katika uzalishaji wa maji.
Aidha pia aliitaka Wizara ya Maji kuhakikisha wakandarasi wanalipwa kwa wakati ili wasikwamishe kasi ya ujenzi wake
Aliongeza kwamba wanamshukuru Rais kwa kutoa kiasi cha Bilionio 35 kwa ajili ya mradi wa Mkinga-Horohoro kupitia fedha za ndani.
Alisema Kamati hiyo inataka kuona mradi huu unakamilika kwa wakati ili ifikapo mwaka 2030 malengo ya Serikali ya kufikisha maji kwa asilimia 100 yawe yametimia.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tanga UWASA, Mhandisi Godfrey Hilly alisema kuwa mradi huo unajumuisha upanuzi wa kituo cha kusukuma maji cha Mabayani kutoka lita milioni 42 hadi milioni 72 kwa siku, na ukarabati wa mtambo wa Mowe utakaofikisha uzalishaji wa lita milioni 60 kwa siku.
Hata hivyo Meneja wa RUWASA Mkoa wa Tanga, Mhandisi Upendo Lugongo alisema mkoa unafikia asilimia 79 ya upatikanaji wa maji,.
Alisema kwa wilaya ya ya Mkinga wakitarajiwa kupanda kutoka asilimia 72.1 hadi 89.03 mara baada ya mradi wa Mkinga-Horohoro kukamilika wenye thamani ya shilingi bilioni 35 utakapokamilika.
Kamati ya Bunge imekagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo ambao katika awamu yake ya kwanza unatarajiwa kuhudumia jumla ya vijiji 17 ndani ya wilaya hiyo.
Mhandisi Upendo alisema mradi huo kwa ujumla umefikia asilimia 65 ya utekelezaji wake. Katika ziara hiyo, Kamati imezindua rasmi upatikanaji wa maji katika Kata ya Mtimbwani, ambapo wananchi wa eneo hilo sasa wameanza kupata huduma ya maji safi ya bomba, ikiwa ni sehemu ya mafanikio ya awali ya mradi huo mkubwa utakaohudumia vijiji 37 utakapokamilika kikamilifu.
Awali akizungumza Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso, alimpongeza mkandarasi wa STC huku akieleza kwamba Serikali itaendelea kusimamia ubora wa huduma na kuwashirikisha watu binafsi katika usambazaji ili kuwafikia wananchi wa vijijini haraka zaidi.
Hata hivyo Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Pius Lyanda, aliishauri Serikali kutenga bajeti maalumu kwa ajili ya kuhifadhi vyanzo vya maji na bwawa la Mabayani ili kuzuia uharibifu wa mazingira unaotokana na shughuli za kibinadamu.
EmoticonEmoticon