
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akizungumza na watumishi Umma wa Halmashauri ya Mji na babati vijijini wakati akiwa wa ziara yake ya kikazi Mkoani Manyara, tarehe 8 January, 2026.

Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (hayupo pichani) wakati wa kikao na watumishi hao, tarehe 8 Januari, 2026 katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Ayalagaya.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Emmanuela Kaganda kwa ziara ya kikazi.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akiwasili katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Babati wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Manyara, tarehe 8 Januari, 2026.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (wa pili kulia) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Emmanuela Kaganda baada ya kuwasili katika Ofisi hiyo iliyopo Mkoani Manyara, tarehe 8 Januari, 2026

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Emmanuela

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (watatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali mara baada ya kikao na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, tarehe 8 Januari, 2026. Wa pili kutoka kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Manyara Bi. Maryam Muhaji.
Na Antonia Mbwambo - Manyara
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray amewataka watumishi wa Umma kutambua wajibu wao katika kutekeleza majukumu ya kila siku ili kufanya kazi kwa uwezo, maarifa na ujuzi walio nao kwa lengo la kuboresha huduma ikiwa ni mojawapo ya njia ya kuwatumikia wananchi kwa ustawi wa Taifa.
Mhe. Qwaray ameyasema hayo tarehe 8 Januari, 2026 Mkoani Manyara wakati akizungumza na watumishi wa umma ngazi ya Mkoa, Halmashauri ya Mji wa Babati na Hamashauri ya Wilaya ya Babati wakati alipokuwa katika ziara yake ya kikazi ambapo ni ziara ya kwanza Mkoani hapo tangu alipoteuliwa tarehe 17 Novemba, 2025 na Mhe Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Amesema Waajiri wote wa Taasisi za Umma lazima waweke kipaumbele katika kushugulikia changamoto zinazowakumba watumishi waliopo chini yao ikiwemo madai ya kupandishwa vyeo na malimbikizo ya mishahara ili kuongeza dhana ya uwajibikaji na kupunguza malalamiko ya watumishi hao.
“Ukiona mtumishi wa umma anakuja hadi Wizarani kwa ajili ya kufuatilia utatuzi wa changamoto zake za kiutumishi, ujue wewe kama msimamizi hujawajibika ipasavyo”,Mhe. Qwaray alisema.
Pia Mhe. Qwaray amewataka watumishi kuzingatia Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma ambazo zinaelekeza tabia na mienendo ambayo mtumishi anapaswa kuwa nayo anapokuwa anatoa huduma katika eneo lake la kazi.
“Mtumishi anapokuwa eneo la kazi hana budi kuachana na masuala binafsi na kujikita katika utoaji wa huduma kwa mwananchi ili kutumia vizuri rasilimali za Serikali katika kuhakikisha kila anayefika kupata huduma anaipata kwa wakati”, Mhe. Qwaray alisema.
Aidha amesisitiza matumizi ya mifumo iliyopo na inayotumika katika kushughulikia masuala mbalimbali ya kiutumishi ikiwemo maombi ya uhamisho na likizo ili kuendana na teknolojia iliyopo kwa lengo la kuwa na utendaji unaozingatia muda na usawa.
Mhe. Qwaray alihitimisha kwa kutoa wito kwa watumishi wa umma kuwa wazalendo na wenye kutanguliza Maslahi ya Taifa mbele katika kulinda na kuimarisha Amani ya nchi kwa kutoa huduma bora, kuzingatia maadili ya kazi na kuepuka vitendo vinavyoweza kuleta mgawanyiko katika jamii.
EmoticonEmoticon