Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso,akizungumza wakati wa Mkutano wa Tisa wa mwaka wa Bodi za Maji za Mabonde nchini uliofanyika leo Januari 28,2026 Jiji la Dodoma.
.....
Waziri Wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amewataka wakurugenzi wa bodi za maji za mabonde nchini kuonyesha umuhimu wa taasisi hizo kwa wananchi kwa vitendo kwa kutoa huduma sahihi.
Waziri Aweso ametoa maelekezo hayo katika kikao cha Bodi za maji za mabonde nchini katika ukumbi wa Jiji la Dodoma.
Aweso ambaye ndiye mgeni rasmi katika kikao hicho amewataka viongozi wa mabonde hayo kutambulika kwa utoaji wa huduma na si kutambulika kwa sifa mbaya kwa wananchi na serikali ikiwemo utozaji wa Kodi zisizi halali.
Aidha Serikali bado inaendelea na mpango mkakati iliyojiwekea katika kujenga mabwawa ya kimkakati kuendelea kupanda miti rafiki wa maji kwa mazingira Ili kuboresha vyanzo vya maji na kutoa huduma ya uhakika kwa wananchi.
Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri amewataka wakurugenzi na wenyeviti wa Bodi za maji za mabonde nchini kuendelea kutunza vyanzo vya maji Ili kuwa na uhakika wa huduma ya Maji kwa mwananchi.
Ameeleza kuwa vyanzo vya maji nchini ni muhimu katika kikao mabonde yanakuwa na maji ya kutosha kutoa huduma kwa wananchi.
Kadhalika Ili kuwe na uhakika wa utunzwaji wa vyanzo vya maji, amezitaka Bodi hizo kushirikiana na jamii na wadau wa mazingira ikiwemo Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI pamoja na taasisi zinazojihusisha na mazingira, Ili kuweka mipango mikakati ya Pamoja katika utunzwaji wa vyanzo vya maji.

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso,akizungumza wakati wa Mkutano wa Tisa wa mwaka wa Bodi za Maji za Mabonde nchini uliofanyika leo Januari 28,2026 Jiji la Dodoma.
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso,akizungumza wakati wa Mkutano wa Tisa wa mwaka wa Bodi za Maji za Mabonde nchini uliofanyika leo Januari 28,2026 Jiji la Dodoma.
EmoticonEmoticon