WANANCHI VUO WAPATIWA FEDHA KUNUSURU RASILIMALI BAHARI

December 07, 2025


‎Na Boniface Gideon,TANGA

‎Wakazi wa kijiji cha vuo wilayani Mkinga mkoani Tanga,wamepatiwa mafunzo ya usimamizi wa mazingira ya Bahari na usimamizi wa fedha ikiwa ni juhudi za kunusuru viumbe Bahari ikiwemo makazi ya samaki ( matumbawe) ,kulinda uvuvi haramu,kutunza fukwe ,upandaji miti ya mikoko pamoja na kulima kilimo cha mwani.

‎Sambamba na mafunzo hayo,wakazi wamepatiwa fedha Sh.10.5 Mil.kwaajili ya kuendesha biashara ili kupunguza utegemezi wa shughuli za baharini,


Fedha hizo ni sehemu ya mradi wa pwani yetu unaosimamiwa na Shirika la Maendeleo la GIZ kwakushirikiana na Shirika la Mwambao Coastal Community Network Tanzania.

‎Akizungumza ,wakati wa hafla ya kukabidhi fedha  kwa Wakazi wa kijiji hicho,Mratibu wa mipango kutoka Shirika la Mwambao Coastal Community Network Tanzania,Abubakar Masoud,alisema fedha hizo zimetolewa kwenye vikundi 5 vyenye wanachama 150 ,kwaajili yakuwasaidia kujikwamua kiuchumi kupitia biashara ili kupunguza utegemezi wa shughuli za kibinadamu baharini,

‎"fedha hizi ,ni sehemu ya mkakati wetu wa kupunguza shughuli za kibinadamu baharini na kuongeza kipato kwa wakazi ,tunatarajia kuona matokeo chanya ya fedha hizi,niwaombe Watu wote mnaokwenda kunufaika na fedha hizi ,mkazitumie kwenye malengo yaliyokusudiwa ili yalete matokeo chanya yaliyokusudiwa "Alisisitiza Masoud


‎Kwaupande wake ,mratibu wa Shirika la Mwambao Coastal Community Network Tanzania mkoa wa Tanga ,Ahmad Salim ,alisema ,kabla ya kutolewa kwa fedha hizo,wakazi wa kijiji hicho walipatiwa mafunzo maalumu ya kuwajengea uwezo kwenye nyanja mbalimbali ikiwamo utunzaji wa mazingira na usimamizi wa fedha,


‎"Kabla ya hatujatoa fedha hizi,tulianza kuwajengea uwezo wa kiuchumi,usimamizi wa mazingira na fedha ,lengo ni kuwafanya wakazi hawa waweze kujisimamia hata sisi tukiwa hatupo,tunaamini Elimu waliyoipata itawasaidia kusimamia utunzaji wa mazingira na fedha,na kila mmoja atakuwa balozi wa mazingira,hivyo niwaombe kila aliyepata Elimu hii akawe balozi wa mazingira ili tutimize lengo" aliongeza Ahmad


‎ MWISHO

Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »