MKUU WA WILAYA KOROGWE AIPONGEZA TAWIRI

December 16, 2025



Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Kamishna Mstaafu wa Uhifadhi William Mwakilema ameipongeza Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) pamoja na Shirika lisilo la kiserikali (Honey Guide) Kwa kuja kutoa mafunzo ya mbinu mbadala za udhibiti migongano baina ya Binadamu na Tembo, hasa wakati huu Wilaya ya Korogwe inapokabiliananna changamoto ya ongezeko la Migongano baina ya wanyamapori na binadamu.

Vilevile amemshukuru Mwakilishi kutoka Shirika la Chakula Duniani (FAO) Beatha Fabian Kwa kuwezesha mafunzo haya ambayo yatakuwa na tija Kwa wakazi wa vijiji vinavyopakana na hifadhi ya Taifa Mkomazi ambavyo vinasumbuliwa mara kwa mara na uharibu na madhara yanayosababishwa na Tembo.

Akifungua mafunzo haya leo tarehe 16.12.2025, kwa wananchi 29 kutoka Kata saba za Mkomazi ambazo ni Mkumbara, Mswaha, Kalalawi, Mkalamo, Mazinde na Magamba na kwalukonge pia amewataka wawakilishi hao kusikiliza kwa makini na kuwa mabalozi wazuri wa kupeleka elimu hii kwa wananchi.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »