WAKANDARASI WALIOSHINDA ZABUNI YA UTEKELEZAJI MRADI WA KUSAMBAZA UMEME VITONGOJI 527 MKOANI TANGA WATAMBULISHWA RASMI

January 30, 2026


Wakandarasi walioshinda zabuni ya kutekeleza mradi wa kusambaza umeme katika vitongoji 527 mkoani Tanga kupitia Kampuni ya Giza cable industries pamoja na Energy service Limited ka wametambulishwa rasmi mkoani Tanga kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi huo

Mradi huo unatekelezwa na Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wenye thamani ya shilingi bilioni 73.8 ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa kuwezesha vitongoji hivyo kuweza kupata nishati hiyo muhimu

Akizungumza wakati wa halfa ya kuwatambulisha wakandarasi hao Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi. Hassan Saidy wakati wa kuwatambulisha Wakandarasi waliuoshinda zabuni ya kutekeleza mradi huo, Kampuni ya Giza cable industries pamoja na Energy service Limited katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.

Alisema wakati wanafanya nao majadiliano kuna maagizo mahususi waliwapa na wangependa kama kiongozi wa mkoa waifahamu ikiwemo kuwaelekeza wawe na timu ya kufanya kazi karibu kila Wilaya.

Aidha aliwataka wakandarasi haoa kujiepusha na vitendo vya kutoa lugha chafu, pamoja na vitendo vya rushwa wakati wanatekeleza miradi hiyo kwa wananchi.

Aliongeza kuwa ukifanya kazi kwenye mradi wa Serikali wanatakiwa kufanya kama mtumishi wa umma hivyo lugha chafu hazikubaliki ikiwemo kurubuni wanakijiji ni kitu ambacho kitapelekea kuvunja mkataba wako.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Dadi Kolimba aliipongeza serikali kwa utekelezaji wa mradi huo na kusema kuwa utakwenda kufungua zaidi fursa za uchumi vijijini.

“Ukiangalia kwa wakandarasi hawa wawili ambao wametambulishwa leo ambao wanaenda kutekeleza mradi wa kupeleka umeme katika vitongoji 527, jumla ya shilingi Bilioni 73.8.

Hata hivyo alisema kwamba wana kila sababu ya kumshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha kutoa fedha za kuwezesha kutekelezwa kwa mradi huu.

Kolimba aliwataka wakandarasi hao kuhakikisha wanamaliza mradi huo ndani ya muda uliopangwa.

Alitoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa wakandarasi hao pindi watakapoanza kutekeleza mradi huo ili malengo yaliyowekwa na serikali yaweze kufikiwa.

Mwisho.









Share this

Related Posts

Previous
Next Post »